2017-09-19 14:13:00

Kard.Ravasi: Lazima kuwa na ujasiri wa kurudia thamani ya historia


Zimekuwa siku nne za makutano na mijadala kati ya mawaziri, wanafilosfia, wasanii, watu wa dini, waandishi wa habari meneja, na watu mbalimbali wa utamaduni wa kuamini na wasio amini. Ni mkutano uitwao Uwanja wa Francisko wenye lengo la majadiliano ya kitamaduni ulio hitimishwa tarehe 17 Septemba 2017 huko Asizi , ukiwa na kauli mbiu njia. 

Ili kuweza kutoa mzani wa mkutano huo wa majadiliano ya kiutamaduni mwandishi wa habari wa Radio Vatican, alipata kuhojiana na Kardinali Gianfranco Ravasi Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni, ambaye amesema, mada ya mkutano huo imejikita katika njia kwa maana ya kutaka kuwa ujasiri wa kurudia kwa upya kuona thamani kubwa ya historia ya maisha yetu. Kwa njia hiyo  kardinali anasema ni kutafuta uzuri na siyo kwa maana ya upimaji lakini pia kama uhalali, wa kueza kuwajibika katika kijamii na utamaduni ambayo ni njia aliyotekeleza Mtakatifu Francisko enzi zake. Halikadhali ni kuweza kuachana na upeo wa mambo madogo na kufanya mambo makuu yenye kuwa na mguso angalau wenye utakatifu. 

Akiendelea kueleza juu ya mkutano huo kwamba; mkutano wa majadailiano ya utamaduni ni matandao sasa ambao umesambaa katika mabara mbalimbali ya dunia, hivyo inabaki msingi unao endelezwa na utashi wa imani ili kuweza kukabiliana na mazungumzo kati ya maono tofauti, lakini pia  utashi wa kuweza kuona upeo zaidi wa mambo kuanzia nini  maana ya uwepo wa binadamu na msingi ya kuishi kwetu.  Mkutano wa majadiliano ya Kidini huko Asizi unajikita kutafakari siyo tu juu ya mada moja bali hata katika masuala mbalimbali yanayoitia wakati wetu, na kufanya mazungumzo tofauti ya upeo mmoja uliokusanyika pamoja hata hivyo ndani  yake nia ni kwanda mbele zaidi ya mgawanyiko, mgawanyiko wa ujuzi na fahamu za kawaida katika nyakati zetu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.