2017-09-18 15:49:00

Wito wa Baraza la Madhehebu ya Kidini nchini Kenya kabla ya uchaguzi Mkuu


Inahitajika kazi kubwa ya uaminifu na uthabiti katika upigaji wa kura za uraisi. Ndiyo wito msingi wa Shirikisho la madhehebu ya kidini nchini  Kenya wakiomba Tume ya uchaguzi  wa rais nchini Kenya ili kuhakikisha usalama na uamanifu  wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 17 Oktoba 2017 . Ameyasema hayo Mkurugenzi mtendanji wa Tume ya Baraza la Kidini nchini Kenya Bwana Francis Kuria  kwamba lazima kuzingatia misingi hiyo katika uchaguzi ujao kwa kuhakikisha kwanza kabisa wanaweka sawa nyumba zao. Uchaguzi wa Rais ulizinduliwa kwa mara nyingine tena mara baada ya Mahakama Kuu kukataa matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti na kushinda  Rais Uhuru Kenyatta aliyekuwa amemaliza muda wake. Kiini cha mzozo huo ni mfumo wa upigaji kura kwa njia ya mtandao wa umeme uliofanywa na Kituo cha Iebc. Pamoja na hayo Mahakama Kuu bado haijachapisha misingi ya hukumu ya kufuta kura, na kwa hiyo ni mapema kuchunguza kushindwa kwa Iebc.

Hata hivyo, hii inakaribishwa na vyama kadhaa kuchunguza taratibu zao. "IEBC," anasema Kuria, wakati huu unaonyesha Wakenya wanaofanya kazi tofauti na lazima kuboresha mifumo yao na miundo mbinu ili wapiga kura waweze kuamini matokeo. Katika suala hili, viongozi wa kidini wataendelea kuzungumza na viongozi wa Iebc kuhakikisha kwamba Wakenya wanafurahia uchaguzi wa uhuru, wa haki na wa kuaminika. Wakati huo huo, mgombea wa urais, Raila Odinga, aliomba kusitishwa kwa Iebc na ukaguzi wa mfumo wa kupiga kura kwa njia ya mtambo wa  umeme. Na kwamba mshikamano wa Odinga ni kwamba imeeleza hatashiriki kura ya Oktoba 17 ikiwa hakuna mabadiliko muhimu yanayotumiwa na sekretarieti ya Iebc.

Kwa upande wa  Baraza  la Maaskofu Katoliki Kenya limewataka wananchi nchini humo kuweka kando tofauti zao ili kwa pamoja waweze kujenga nchi yao.Baraza la Maaskofu Kenya limekishukuru Chama cha upinzani cha NASA kwa kufikisha malalamiko yake ya uchaguzi kwenye Mahakama kuu badala ya kesi hiyo kusikilizwa na kutolewa hukumu na raia mitaani, hali ambayo ingepelekea machafuko makubwa ya kisiasa nchini Kenya.Uamuzi huu umeiongezea Mahakama kuu sifa ya kuweza kutatua migogoro ya wananchi katika hali ya usalama na amani. Maaskofu wanawaalika wananchi wote wa Kenya kuzingatia utawala wa sheria kwa kukubali na kutekeleza maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kuu. Uhuru, heshima na haki ya Mahakama kuu vinapaswa kuheshimiwa hata kama kimsingi mtu hakubaliani na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kuu.

Maaskofu wanampongeza Jaji Mkuu David Maraga kwa maamuzi aliyoyafanya na kwamba, sasa changamoto iliyoko mbele yao ni kushikamana ili kujenga taifa kwa kujikita katika nia njema. Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawasifu na kuwapongeza wananchi wote waliojitokeza kupiga kura, kwa amani na utulivu na kuwataka tena kujitokeza kwa wingi wakati wa kupiga tena kura ya marudio hapo tarehe 17 Oktoba 2017. Wananchi wa Kenya wanahimizwa kufanya kampeni za kistaarabu, zinazowajibisha, ili hatimaye, kuwapata viongozi watakaosukuma mbele gurudumu la maendeleo ya wananchi wote wa Kenya. Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya wanawaalika  vyama vyote kushirikiana na Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, IEBC sanjari na kuiachia uhuru wa kuweza kutekeleza majukumu yake pasi na kuingiliwa na wanasiasa.

Badala ya kuishambulia Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya, wanasiasa watoe ushauri wa namna ya kuboresha utendaji wao wa kazi na kwamba, busara haina budi kutumika kwani si mambo yote yanaweza kufanyiwa marekebisho. Maaskofu wanaunga mkono mchakato wa mabadiliko kwenye Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, IEBC ili kuwajengea wananchi imani katika mchakato mzima wa uchaguzi wa marudio hapo tarehe 17 Oktoba 2017.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.