2017-09-18 15:07:00

Hati ya utambuzi wa Utakatifu wa Mtumishi wa Mungu Kard. Van Thuân


Misa ya shukurani imeadhimishwa huko Roma katika Kanisa la Mtakatifu Maria kutokana kutambuliwa  Hati ya karama za kijasiri za utakatifu wa Kardinali François-Xavier Nguyên Van Thuân na  kukubaliwa kuitwa mtumishi wa Mungu. Hati hiyo imetolewa kwa wote katika Lugha ya Kiitaliano na lugha ya Kivietman katika maadhimisho yaliyoendeshwa na Kardinali Peter Turkson Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo ya mwanadamu, ambaye ndiye anashughulikia mchakato wa kutangazwa mwenye heri.

Katika maandishi ya mtumishi wa Mungu  anasema, mbegu kuanguka ardhini na kufa siyo tu njia ya kuzaa matunda, bali hata kuokoa maisha binafsi, kwa maana ya kuendelea kuishi.Hiyo ndiyo njia fasaha ya kuelezea njia ya Maisha, Kardinali Turkson akikumbuka maisha yake na kwamba ndiyo maana ya  uchaguzi wa wito wake  kikuhani. Aidha mtindo wa utakatifu wake wakati wa kuishi ulitokana na kuiga mifano ya baadhi ya watakatifu kama vile Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu kupitia katika tasaufi ya utoto wake; ya Mtakatifu Yohane Maria wa  Vianey, aliyemfundisha karama ya utii, uvumilivu na thamani kuwa na jitihada, pamoja na Mtakatifu Francisko Xavier, Mtume mkubwa anayejulikana katika Bara la  Asia ambapo alijifunza kutoona fahali mbele ya mafanikio au kushindwa.

Jitihada za utume  wa Mtumishi wa Mungu uliendelea na ujio wa tukio la utawala wa Kikomunisti. Baadaye akakamatwa kwa mashtaka ya kwamba ana njama kati ya Vatican na watawala wa Vietnam  mnamo tarehe 15 Agosti 1975, katika Sikukuu ya Kupalizwa Mbinguni Mama Maria. Kwa njia hiyo, Kardinali Turkson anarudia kuelezea historia yake wakati yuko  kifungoni kwa  kutengwa kwa kipindi cha miaka kumi na tatu, mpaka 21 Novemba 1988. Alijaribu kuishi maisha ya gereza kwa kutulizwa na upendo, kama vile ushuhuda wa imani, matumaini na upendo wa Mtumishi wa Mungu, ambao ulisambaa siku hadi siku, kwa unyenyekevu na busara. Na hiyo ni mwaliko  daima wa utakatifu ambao unapata kujieleza  kwa uaminifu kwa Mungu na kwa msaada wa kufuata njia ya utakatifu.

Kardinali Turkson akifuata matukio binafsi ya mtumishi wa Mungu hadi kufikia  katika hati ya hiyo ya utambuzi wa matendo ya utakatifu, pia anasisitiza hata mtazamo wake wa upole, uvumilivu na upendo kwa jirani, ambao uliwafanya wafungwa wenzake na hata wanafunzi wake kusikiliza Neno la Mungu na kwa njia hiyo Kardinali Turkson anatoa wito kwa jumuia nzima ya Wakristo kuiga mfano huo wa mtumishi wa Mungu Xavier Nguyên Van Thuân. Kwa maana katika kipindi chote cha kifungo katika magereza, upendo wa Yesu msulibiwa na kujikabidhi ndivyo vilikuwa ufunguo wa maisha yake.

Ikumbukwe kabla ya Conclave ya uchaguzi wa Papa mwaka 2013 , ilitungwa sala ya kuombea uchaguzi huo kwa kwa kupitia maombi ya  Kardinali Nguyen Van Thuan sala hiyo ilikuwa inasema: Ee Mungu, Baba yetu wa Mbinguni, kwa maombezi ya mtumishi wako mwaminifu, François Xavier Nguyen Van Thuan, tujalie kuwa na hekima ya Roho Mtakatifu katika uchaguzi wa Baba Mtakatifu mpya, atakayekuwa "Mtumishi wa Watumishi wa Mungu," na mwenye upendo mkamilifu katika kulitumikia Kanisa lako kwa uaminifu. Tunaomba hayo katika jina la Yesu Kristo Mwokozi wetu, anayefungua mioyo yetu tupate kukujua, kukupenda na kukutumikia Wewe kwa uaminifu. Amina

Historia ya Kardinali François Xavier Nguyen Van Thuan

Kardinali, Van Thuân alizaliwa nchini Vietnam tarehe 17 Aprili 1928, katika familia yenye msingi ya kikatoliki na kupata daraja la upadre tarehe 11 Juni 1953.  Aliteuliwa kuwa Askofu wa Nha Trang, tarehe 13 Aprili 1967, na mwaka 1975  akateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Saigon.
Baada ya siku mbili tu akakamatwa na polisi na kutumikia kifungo cha mika 13 , miongoni mwa miaka hiyo, miaka 9 alitengwa peke yake. Aliachiwa huru tarehe 21 Novemba 1988. Tarehe hiyo inakumbukwa na Kanisa Katoliki kuwa siku Mama Maria kupelekwa Ekaluni ambapo katika maandishi ya Kardinali Van Thuan anasema, kuachiwa kwa sambamba ya Siku kuu ya mama Maria inampa uhuru.

Mwaka 1998 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la haki na Amani ambalo sasa limebadilishwa kuwa ni Baraza Kipapa la Huduma ya Maendeleo ya Watu na Mwenyekiti wake ni Kardinali Peter Turkson ambaye anaendesha mchakato wa kutangazwa mwenye heri. Aidha aliteuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili kuendeleza mafungo ya kiroho mwaka 2000 Vatican, wakati wa kutoa mafungo hayo, papa alimwelezea kuwa "aliishi maisha yake kwa hekima na ujasiri kwa wito wake”. Wakati huo huo Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa katika Baraza la Makardinali tarehe 21 Februari 2001. Bwana Mungu akamwita kwakwe tarehe 16 Septemba 2002 akiwa na umri wa miaka 74 kwa ugonjwa wa Salatani. Mazishi yake yalikuwa ni tarehe 29 Septemba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , ambapo liturujia ya mazishi iliongozwa na Matakatifu Yohane Paulo II na  mahubiri, wakati Liturujia ya ekaristi iliadhimshwa na Kardnali Angelo Sodano aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vatican wakati huo.

Tarehe 6 Juni 2012 Masalia yake yalihamishwa kwa ibada maalumu na  Kardnali Peter Turkison,na  kupelekwa katika Kanisa la Mtakatifu Maria wa Scala , Kanisa ambalo alikuwa amekabidhiwa  kwa heshima ya kuwa katika Baraza la Makardinali Roma. Tangu tarehe 22 Oktoba 2010 ulifunguliwa rasmi mchakato wa kutangazwa mwenye heri katika ukumbi wa Laterano mjini Roma uliyo wakilishwa na Mnetherland Waldery Hilgeman, mwandesha hoja za  usajili wa mchakato. Lakini kufunguliwa kwa mchakato huo haukupokelewa vema na Serikali ya Vietinam kutokana na kwamba alikuwa amehukumiwa na kufungwa Kardinali huyo. Na hivyo inakumbukwa kwamba hata serikali ya Vietinam hakuweza kumpatia ruhusa mzalendo wake aliyekuwa afike Roma kwa ajili ya kutoa ushuhuda wa Kardinali Nguyên Van Thuân.

Tarehe 5 Julai 2013 ilihitimishwa  sehemu ya mwisho ya jimbo kwa ajili ya mchakato huo na wakati wa tukio hilo, Kardnali Agostini Vallini aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Roma alielezea kuwa mtumishi wa Mungu Van Thuán  alikuwa kama bingwa halisi wa Injili hai. Tarehe 4 Mei 217 Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu ilimaliza mchakato wa kutangazwa Mwenye heri na kutambua  karama zake za ujasiri wa kushuhudia Injili. 

Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.