2017-09-16 17:04:00

Ujumbe wa Papa kwa Washiriki wa Hija ya Familia Kitaifa Italia


Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Septemba 2017 kwa ajili ya washiriki wa Hija ya 10 Kitaifa ya familia kwa ajili ya familia katika Madhabahu ya Mama Maria wa Pompei, iliyoandaliwa na Baraza la kipapa kwa ajili ya familia na maisha, vyama vya kitume na taasisi za Kitaifa katika utume wa kichungaji wa familia wa Baraza la maaskofu nchini Italia.  

Ujumbe wake ulio tiwa saini na Kadinali Petro Parolin , Baba Mtakatifu Francisko anawatakia matashi mema na uwepo wake karibu kiroho. Pia anafurahishwa na tukio hilo la kila mwaka, lakini zaidi katika mwaka huu ambapo ni katika mtazamo wa maandalizi ya Siku ya Familia duniani itakayofanyika huko Dublin 2018. Zaidi Baba Mtakatifu anawataka wasali kwa ajili ya familiza zilizojaribiwa katika ukosefu wa ajira, wale wanaoteswa kwa ajili ya imani yao na kwa ajili ya kila familia katika hali ya mateso. 

Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Italia, Askofu Mkuu Nunzio Galantino ameongezea ujumbe wake kwa Mwenyekiti wa Chama cha Uamsho wa Kikatoliki Bwana Salvatore Martinez. Akisisitiza juu ya thamani  ya kushuhudia hija iliyofunguliwa kwa wote anasema, ni tunu msingi ya kuleta umoja katika maombi na kukumbusha juu ya nafasi ya familia ya leo katika mantiki ya kijamii, elimu ya binadamu na utaifa. Askofu Mkuu Galantino anasema, siyo rahisi kutoa ushuhuda wa wema, uaminifu na matumanini katika nyakati hizi ambazo familia nyingi zinapitia katika kipeo  kikubwa mafundisho ya kibinadamu, uchumi, kijamii na  mambo mengi yanayoleta mgawanyiko ndani ya familia, pia umaskini. Pamoja na hayo bado kuna changamoto ya  woga wa kutamka  “ndiyo daima” kwasababu ya changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa ajira,dharura za umma katika nchi ambayo haitoi nafasi ya kwanza ya familia. Kwanjia hiyo vijana wanashindwa kuunda familia na kusabisha upungufu wa kizazi na kupunguza ndoto hizo za vijana, na matotokeo ni idadi ya watu kupungua .

Halikadhalika Askofu Mkuu anatoa masikitiko ya sasa ambayo anasema, kwa bahati mbaya, taasisi nyingi zinaonekana kutojali na kukubali ukweli na umuhimu wa msingi wa familia, ya kwamba  inaundwa na muungano wa mke na mme, badala yake ni kile kinachooneka wazi kwa upinzani ambao umeenea na kubaki  mahali ambapo wengi wanataka kuinamia kwa siku zijazo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.