Ni karibia asilimia 75 ya kazi ya kuchunguza Katiba ya mwongozi wa Kitume Vatican na mwisho wa mwaka huu kutakuwapo na uwezekano wa kuwasilisha nyaraka mpya kwa wanasheria wa Vatican. Ameyathibitisha maneno hayo katika vyombo vya habari vya Radio Vatican Kardinali Óscar Andrés Rodríguez Maradiaga, Askofu Mkuu wa Tegucicalpa (Honduras) ambaye ni Mratibu wa Baraza la Makardinali washauri wa Papa wakati wa kumalizia Mkutano wa 21 wa baraza hilo.
Shughuli za kitume katika mkutano huo si kwa ajili ya Baraza la Makardinali tu, bali pia ni lazima kujibu malengo ambayo Baba Mtakatifu Francisko amekabidhi.Kati ya masuala muhimu aidha amesema kuwa wanaamini kwamba baba Mtakatifu anayo matashi ya kutaka kuongeza zaidi wanawake na vijana ndani ya utume Vatican.Halikadhalika miongoni mwa mada zilizo jadiliwa katika Baraza hili jipya ambalo ni kama chombo cha uinjilishaji na huduma ambayo si kwa ajili ya Papa bali hata kwa ajili ya Makanisa mahalia ilikuwa: ugawaji wa madaraka, nafasi ya ubalozi wa Kitume, uteuzi na uwezo wa wafanyakazi, ambao wanapendelea wau wa kanisa wawe wachache zaidi lakini kuwajumuisha na wengi wa Kimataifa.
Naye Askofu Marcello Semeraro wa jimbo la Albano, nchini Italia ambaye ni Katibu
wa Baraza la Makardinali washauri wa Papa anathibitisha hayo kuwa mchakato wa mageuzi
ya Vatican umefikia sasa zaidi ya robo tatu na inatayarishwa kwa kiwango cha pendekezo
la Baba Mtakatifu. Mkutano wa Baraza la Makardinali washauri wa Papa utafanyika tena
tarehe 11-13 Desemba 2017.
Naye Mkurugenzi wa Habari za Vatican Bwana Greg Burke ametoa habari zaidi juu ya
Mkutano wa 21 wa Baraza la Makardinali washauri. Anasema Mkutano ulifunguliwa tangu
jumatatu, kwa siku tatu uliudhuliwa na wajumbe wote japokuwa Kardinali George Pell
na Kard. Laurent Monsengwo Pasinya hawakuwapo.
Akiongea na waandishi wa Habari, Bwana Burke ameweka bayana kuwa, Baba Mtakatifu
ameshiriki na kundi hili kuanzia Jumanne asubuhi mara baada ya kutoka katika ziara
yake ya kitume nchini Colombia, na hakuweza kuwapo Jumatano asubuhi kutokana na shughuli
ya Katekesi yak ila Jumatano.
Kwa njia hiyo anasema, shughuli za Mkutano huo zilikuwa ni juu ya kusoma na kutafakari
mapendekezo ya Baba Mtakatifu aliyotoa kwa Baraza hilo jipya. Pamoja na hayo kulikuwa
na tafakari iliyoongozwa na Kardnali Óscar Rodriguez Maradiaga Mratibu wa Baraza hilo,
kuhusiana na nyaraka mbalimbali za Papa juu ya mageuzi. Na hizo nyaraka hasa ni zile
zitotokanazo na Mkutano wa jadi wa Papa na Jumuiya nzima ya Vatican aliotoa hotuba
wakati wa kutoa matashi mema ya Krismasi, hotuba nyingine za mkutano Mkuu tarehe 12
Februari 2015, na 17 Oktoba 2015 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Sinodi ya Maakofu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |