2017-09-15 16:31:00

Simikeni mizizi ndani na kubaki kidete juu ya mwamba wa Yesu


Somo la kwanza kutoka  katika barua ya wakolosai, inatoa fursa ya kuonesha wazi maisha yetu ya kikristo. “Kwamba maadamu nyinyi mmekubali Kristo Yesu aliye Bwana, basi ishini katika muungano naye muwe na mizizi ndani yake mjijenge juu yake na kuwa  imara katika imani kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrni tele”. Kwa njia hiyo kumfuafa Yesu, siyo jambo la wito wa furaha ya siku moja tu, au kwa kipindi fulani,au fursa za ushuja , hili ni tendo la kukubali kabisa kila siku,kujikita kujibu kwa dhati ile ndiyo na  kuwa mfuasi wa Injili,  mhudumu na shuhuda wa huruma, kuacha utengezwe naye kwa upya umfuate, na kumtambua kama ni mwanakondoo wa Mungu.

Ni tangulizi wa mahubiri yake Monsinyo Dario Vigano Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican wakati wa ibada ya misa kwa washiriki wa mafunzo yalikuwa kuwa na kauli mbiu zawadi ya utawala: huduma kwa ajili ya wema ya wote  mapema wiki hii.
Mosninyo anasema, mtume Paulo anatumia maneno wazi  kiasi cha kuonesha tabia za kufuasa. Kwa maana ya  tembeeni kwasababu imani ya kikristo siyo ya kukaa kaa tu, kama wale wanao kaa katika sofa na kusubiri, bali ni wale ambao wanajikita kwa undani kutoka nje na kuanza kufanya hatua ya kwanza, kutafuta, kukutana,na hata kama hiyo inawalzimisha warende katika sehemu ambazo hazikubaliki kama vile vijini na pembezoni kwa ajili ya ndugu kwa mijibu wa wito wa Baba Mtakatifu Francisko.

Akieleza zaidi, anaendelea kutumia maneno ya Baba Mtakatifu Francisko anayetoa wito kuwa, Bwana hataki kuona watu wake wanatembea nyuma yake bila kuwa na utashi, bila kuwa na chembe  kidogo ya furaha katika mioyo yao. Yesu anataka kuona watu waliofanya uzoefu naye  wamepokea furaha isiyo kuwa na kifani , na furaha hiyo inageuka kuwa furaha na ushuhuda kila. Mfuasi wa Ufalme wa Mungu asiye kuwa na furaha katika ulimwengu huu ni mwenye huzuni.  Na huyo wakati mwingine aweza kuwa muhubiri wa Yesu kwa mabawa ya maneno tu , kwa maana anaweza kuonge sana tu lakini hakuna la maana. Je unawezekanaje kuwa mtangazaji wa Neno la Yesu?. Ni kwa njia ya kuonesha furaha ya kweli kwa wale wamchao Bwana. Na ndiyo maana anasema wanaonekana hata watu kati yetu ambao wanaonesha kweli na kusambaza furaha na imani yao katika macho yao.( Katekesi ya Papa tarehe 30 Agosti 2017).

Monsinyo Vigano anasema, ni lazima kutoa mtazamo wetu na kusambaza furaha ya kwamba umekutana na Bwana, amekuwa kiini cha maisha yako, wakati huo huo ukifanya jitihada za kubaki umesimika mizizi kwake Yeye ambaye ndiyo mjenzi wa utambulisho wetu wa Kikristo juu ya mwamba wa imani kwake na siyo katika mchanga wa kujidanganya kwetu. Akichambua Injili iliyosomwa anaeleza kuwa, Bwana Yesu alikwenda kusali usiku mzima , akitafakari na baba yake, kabla ya kuchagua mitume wake, ambapo baadaye aliwakabidhi utume huo ili watagaze  Injili hadi miisho ya dunia. Muinjili Luka anaonesha kwamba sala ndiyo msingi wa kila hatua yoyote ya uchaguzi na matendo yake ya kitume ya Yesu,  kwa njia hiyo ndiyo njia ambayo hata Kanisa na kila mmoja analazimika kufanya.

Pamoja na hayo mantiki ya kibinadamu na kufuata maelekezo hayo unaweza kufikiria kuwa uchaguzi huo haukuweza kufanikisha.Lakini tangu mwanzo wa jumuiya ya kikristo ulijionesha sura ya ushuhuda lakini pia giza kutokana na usaliti na kukataliwa. Kwa maana nyingine Petro na Yuda ni sura mbili zinazonesha hali hiyo: Japokuwa tendo hilo linatufanya tutambue kwamba siyo mikakati ya kibinadamu inayoongoza hatua za Kanisa ,bali ni kwa msaada wa nguvu za Roho Mtakatifu, ukarimu wa Baba wa huruma ya mwanae ambayo bila kuchoka  kwa ajili  inaendelea kusaidia  sisi na kuponya majeraha yetu, kusamehe dhambi zetu , kufunga madonda na kufanya ujenzi wa  kuunda upya yote yaliyochakaa  kwa kuanza maisha mapya. Kwa njia hiyo tunaweza kuimba kwa pamoja zaburi isemayo: Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma na rehema hakasiriki ovyo amejaa fadhili. Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wote, ni mwenye huruma kwa viumbe vyake vyote. (Zab144/145,8-9) Kwa matazamo huo na zoezi la karama  hizo zinaweza kuwafanya kuishi kwa pamoja, japokuwa na karoro na madhaifu ya kila mmoja lakini kwa kushirikisha kwa pamoja na kuishi kindugu.
Sr Angela Rwezaula


Idhaa ya Kiswahili ya Radio.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.