2017-09-11 14:58:00

Papa Francisko:Katika vurugu hizi utafikiri hakuna njia za amani


Kuanzia tarehe 10 hadi 12 Septemba huko Osnabruk Ujermani unafanyika Mkutano kuhusu njia za Amani. Ni mkutano wa Kimataifa ulio andaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio juu ya tasaufi ya Assizi. Ni chama cha mazungumzo kati ya dini za ulimwengu na tamaduni, kilichoanzishwa mara baada ya  tukio la kihistoria la Siku ya Maombi ya Amani iliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II Oktoba 1986. Mkutano huo unaudhuliwa pia na Cansela Angela Merkel wa Ujermani. Eneo ambalo limechaguliwa kufanyika tukio hilo la mkutano huo huko Westphalia linakumbusha mahali ambapo, mwaka 1648, walitia saini ya makubaliano ya amani na mwisho wa kile kinachojulikana kama vita ya miaka thelathini, aidha kutaka  uwepo wa heshima na utambuzi wa madhehebu madogo ya kidini barani Ulaya.

 Katika tukio hilo, Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa wawakilishi wa mkutano huo wa kimataifa akisema, Munster ndipo mkutano unaendelea wa safari ya amani na mazungumzo  yaliyoamzishwa na Yohane Paulo II huko Assizi 1986. Anaelekeza umuhimu wa sasa katika njia za amani ambayo ni kauli ya mkutano kwamba ni njia ambazo  ni sambamba na njia zilizochukuliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, mbele ya migogoro na vurugu zilizosambaa kila mahali, ugaidi na vita ambavyo leo hii ni tiishio la mamilioni ya watu wanaodhaurauliwa  na kukanyagwa maisha yao kama binadamu  hasa wadhaifu na waathirika.

Kulingana unaoudhuliwa na viongozi wa kidini, hata kisiasa na utamaduni kutoka mataifa mbalimbali ya ulimwengu huu, wakijadiliana kwa pamoja  ili kutafuta njia  mwafaka  za pamoja na mbadala dhidi ya vurugu na vita, lakini pia umaskini na matatizo ya kijamii, kwa lengo la kutafuta njia mpya za kukabiliana, Baba Mtakatifu anaandika kuwa, utafikiri vurugu hizi hazina njia ya kutokea, ni mahali ambapo hakuna anayetaka kuchukua njia za maridhiano. Ni mahali ambapo wanaamini  katika nyenzo za siraha  kuwa suluhisho kwa kudharau  mazungumzo na kuacha  watu wengi katika usiku wa giza la vurugu na ghasia , bila matumaini ya machweo ya amani.

Baba Mtakatifu Francisko anawaelekeza kwamba, majibu kwa wale ambao wana kiu ya amani lazima yawafikie wale wanao wajibika kama vile viongozi wa kisiasa  na kiraia, lakini hasa zaidi kwa viongozi wa kidini ambao wanaalikwa  kwa njia ya maombi, kujibidisha kwa dhati, kwa unyenyekevu katika  ujenzi na kujibu kiu hii ya watu kwa kuwatambua na  kufungua njia za amani bila kuchoka.  Mbele ya kipeo cha upungufu wa njia hizo anasema, wale wanaomdharau Mungu na kupandikiza chuki , katika uso wa vita,  katika wenda uzimu wa ugaidi, na nguvu za udanganyifu wa silaha, ni dhahiri kwamba haiwezekani kupata njia za amani, kwa njia hiyo ni ombi la Baba Mtakatifu kuwa, inahitajika  ujasiri, unyenyekevu na uvumilivu ili kutafuta njia za amani na hasa kwa sala za dhati ambazo ni mizizi ya amani.

 
Hawali ya yote Baba Mtakatifu anasema, ni kwa viongozi wa kidini ambao wana jukumu  kwanza kuwa na uzoefu pia kuishi kama watu wa amani, kushuhudia kwamba Mungu huchukia vita na   kwamba kamwe vita haziwezi kuwa vitakatifu  wala jeuri la vurugu haliwezi kamwe kuhesabiwa haki kwa jina la Mungu. Na hiyo siyo rahisi kubaki tofauti mbele ya matukio haya ya kuhatarisha. Maana  matukio hayo yanaangukia katika chuki na binadamu ambaye hawezi kujitoa katika shida hizi kwa mawazo ya kwamba binadamu amewekwa pembezoni na kuzidi kunyanyaswa kwa mabavu na kunyonywa.
Kwa  hiyo Baba Mtakatifu anasema mkutuno wa Munster uwe ni fursa ya kushinda utofauti wa kutokujali mbele ya mateso ya wanadamu, kwa  kutafuta  njia za  kujikomboa na maovu ya vita na chuki licha ya tofauti hizo za kutokujali zilizopo. Hiyo ni kwamba kamwe maovu yasiwe ya kawaida na kamwe pasiwepo na ubaguzi, na wala chuki ya mt una mtu mwingne bali umoja wa kukutana na upendo. 

Kwa kumalizia Baba Mtakatifu Francisko anakumbuka Mkutano wa Ulaya wa  katika madhimisho ya miaka 60 ya mkataba wa Umoja wa nchi za Ulaya kwamba, waweze kukuza amani katika ujenzi wa njia zaidi na thabiti ndani, zaidi katika ufunguzi wa milango ya nje, kwani wasisahau kuwa amani siyo tunda la juhudi ya binadamu tu bali ni kufungua hawali ya yote  wazi kwa Mungu. “Tuendelee  kufungua pamoja njia mpya za amani. Taa za amani zinawaka mahali ambapo kuna giza la chuki. Ni lazima pakawepo utashi kwa upande wa wote ili kuweza kuondokana na vikwazo vinavyogawanya, ili kuweza kukuza vifungo vya ushirikiano binafsi vya upendo, kuwaelewa wengine, kuwasamehe wale wanaotesa  ili watu wote duniani waweze kuwa ndugu na kustawi na kutawala amani daima”

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.