2017-09-10 15:57:00

Askofu mkuu Pioppo ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Indonesia


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Mkuu Piero Pioppo kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Indonesia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Piero Pioppo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Cameroon na Equatorial Guinea. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Poppo alizaliwa tarehe 29 Septemba 1960 huko Savona, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 29 Juni 1985 akepewa Daraja Takatifu ya Upadre. Amebahatika kuwa na Shahada ya Uzamivu katika Mafundisho Sadkifu ya Kanisa.

Askofu mkuu Pietro Pioppo alianza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Vatican kunako mwaka 1993. Tangu wakati huo, ametekeleza dhamana na majukumu yake katika Balozi za Vatican nchiniKorea, Chile na kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican, akishughulikia masuala ya huduma za jumla. Kunako mwaka 2010 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Cameroon na Equatorial Guinea.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.