Katika tukio la ufunguzi wa Mkutano wa XXV wa Kimataifa wa Kiekumene wa tasaufi
ya Kiorthodox, napenda kuwasalimia waandaji na washiriki wa Mkutano huo. Ni maneno
ya utangulizi wa Baba Mtakatifu alio utuma Enzo Bianchi Mwanzilishi na Mkuu wa Jumuiya
ya Wamonaki wa Monasteri ya Bose, ambao wameanza mkutano wa XXV wa kimataifa wa tasaufi
ya Waorthodox kuanzia tarehe 6 – 9 Septemba 2017 ukiwa na kauli mbiu “Ni zawadi kukuaribisha”.
Katika maneno ya Baba mtakatifu amemsalimia yeye binafsi na kwa namna ya pekee kiongozi
wa Kiekumeni Patriaki Bartholomew na Theodros Patriaki wa Alessandria. Amesema uwepo
wao ni muhimu katika Mkutano huo wa 25 katika Jumuiya ya Wamonaki Bozze kwa ushirikiano
wa Makanisa mengine ya Kiorthodox ambayo inatoa thamani na mchango wa pamoja katika
safari kuelekea katika umoja.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “ni zawadi kukaribisha” kwa njia hiyo inatia
moyo na matumaini hasa katika hali ya sasa .Hakika kukaribisha ni zawadi; ni zawadi
hawali ya yote tuliyoipokea pia sisi wote ni wageni katika ulimwengu, sisi tulio
umbwa na tunaopaswa kulinda. Pia sisi ni wasafiri katika ardhi hii na wageni wa ardhi
hii; kwa njia kama ni wageni tunalikwa na kutarajiwa huko mbinguni, mahali ambapo
kuna uraia wetu (Fil 3,20).
Baba Mtakatifu anasema,wakati huo sisi kama wafuasi wa Emmau tunalikwa kutazama mahali
ambapo hakuna machweo, mahali ambapo upendo hautakuwa na kikomo, mahali ambapo tutapokelewa
mmoja na mwingine kama zawadi ya Bwana kwasababu ya kutakiana mema na upendo, hurumana
vilevile ma kushiriki uchungu na wale ambao wanateseka tukifikiria kuwa uchungu na
majanga yao ni yetu pia.
Baba Mtakatifu Francisko anatoa wito huo kuwa usikilizwe kwa unyenyekevu katika tafakari za siku hizi za kwenye mkutano wao ili waweze kukua daima na mawazo ya kindugu, kukomaa kwa dhati katika kukaribisha kwa moyo kwa maana wote ni mahuji kuelekea katika ufalme. Pamoja na hayo ni kusukumwa na hatua hizo kwa ujasiri na dhati kuelelea katika umoja wa kweli. Mwisho amwabariki na kuwatakia mema katika mkutano huo wakiongozwa na mapaji ya Roho Mtakatifu na kuwaomba sala zao kwa ajili yake.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |