2017-09-02 17:08:00

Papa:Nishati endelevu ni wajibu wetu na isiwe chanzo cha migogoro


Ninayo furaha ya Onesho la Kimataifa huko nchini Kazakhstani lenye kuwa na kauli mbiu “Nishati endelevu. Ni maneno asemayo Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wa Siku ya Vatican katika Banda la Expo 2017 Astana nchini Khazakhstan. Amewasalia wote walioudhuria katika Siku ya National Day ya Vatican kwenye banda  lililoandaliwa kwenye Onesho la Expo 2017 Astana, wote ambao kwa namna moja au nyingine wametipitia ikiwa ni idadi kubwa ya wengi wanaofanya matembzi katika Onesho hilo. Anasema kwa kauli mbiu “Nishati endelevu, ni muhimu kutafakari  uzito na wajibu juu ya njia ambazo katika miaka ijayo binadamu  atatumia teknolojia mpya na ubunifu wa rasilimali za nishati ambazo zimepokelewa kama zawadi na urithi wa pamoja.

Sisi sote tunatambua hili kwamba namna ya matumizi ya nishati yanategemea sana kwa upande wa afya zote zinazoishi ndani ya  sayari hii na ustawi wa jamii zetu vilevile  kuwa na uwelewa kwa njia muhimu ambazo  siyo tu za ustawi wa kiuchumi au uwezo wa matumizi. Lazima kuhakikisha kuwa nishati inawekwa katika huduma ya kile kinachotufanya kuwa bora zaidi, kile kinachofanya kuchanua na kutoa matunda ya ubinadamu mbapo kwa asili yake huleta uhusiano na wengine, kuelekea umoja na katika upendo. Kwa hiyo, rasilimali za nishati hazipaswi kuwekwa kushoto katika udhanganyifu na wala kuwa chanzo cha migogoro. Ili kufikia lengo lake  tunahitaji mazungumzo  ya kweli  na dhati katika ngazi zote katika sekta mbalimbali za jamii zetu. Nishati endelevu siyo kazi tu kwa ajili ya watafiti, teknolojia na wawekezaji: hata ulimwengu wa utamaduni, siasa, elimu na dini wote wanaalikwa.

Aidha Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa anapozungumza na wao hasa walioko huko, hawezi kutokufikiria utaratibu wa mazungumzo na mashauriano kati ya dini ambayo ni muhimu katika nchi iliyo na utajiri mkubwa wa makabila utamaduni na kiroho.Kwa njia hiyo ni matumani yake kwamba dini mbalimbali katika mazungumzo hayo kwa namna ya pekee anakumbuka hati wosia wake wa Sifa kwa Bwana isemayo maandiko ya dini yanaweza kutoa maana kwa miaka yote, kwani yanayo uwezo na nguvu za kuhamasisha na kufungua upeo mpya(….).Misingi ya maadili yenye uwezo wa kutambuliwa, inaweza kuonesha daima njia tofauti na kuelezwa kwa lugha mbalimbali hata kidini.

 Kwa hiyo Baba Mtakatifu anasema ni muhimu kwamba kila mtu agundue lengo na misingi ambayo inafanya uwezekano wa kuhimiza au kuhamasisha ujasiri wa kuboresha na kuvumilia na kuishi pamoja kama ndugu.Mungu mwenyezi asaidie kupata mafundisho ya Expo 2017 na maelekezo ambayo yadumu kwa muda mrefu. Amehitimisha kwa kubariki safari ya pamoja katika kutekeleza na kufika maelengo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.