2017-08-31 14:30:00

Papa Francisko akutana na wajumbe wa Jumuiya ya Wayahudi


Ninatoa salam zangu kwa furaha kubwa kwenu ninyi  kwa namna ya pekee kwa wawakilishi wa Baraza la Wakuu wa Jumuiya ya wayahudi wa Ulaya,Marekani na Tume ya Kiyahudi ya Israeli katika mazungumzo na Tume ya  Mahusianao ya Kiyahudi na Vatican.
Ni utangulizi wa salama zake Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hotuba yake mjini Vatican asubuhi ya terehe 31 Agosti alipokutana na wawakilishi wajumbe katika Mkutano wayahudi. Katika safari ya pamoja ansema,  shukrani kwa utashi  ambao unaendelea katika njia ya mazungumzo. Kwa namna ya pekee katika Azimio la Yerusalem na Roma ambapo wamefanyia  kazi na leo amepokea hati hiyo mikononi mwake.

Ni maandishi ambayo hutoa utambuzi wa pekee kwa Azimio la mapatano ya Waraka wa (Nostra Etate)  ambao katika sura ya nne unawakilisha kwetu sisi (magna carta) mwongozo wa  majadiliano na ulimwengu wa Kiyahudi . Kwa njia hiyo utekelezaji wake na  maendeleo unaruhusu mahusiano kuwa zaidi na zaidi ya urafiki wa kindugu. Waraka wa Notra Etate umefafanua katika mwanga na kuonesha mwanzo wa imani ya kikristo ambayo tayari umekuwapo kwa mujibu wa fumbo la wokovu kuanzia baba wa imani , Musa na Manabii ambao pamoja na kuwa na urithi  mkubwa wa kiroho tulionao, ni lazima kuukuza kati yetu na kuwa na utambuzi wa pamoja, zaidi kujikita kwa pamoja kwa njia ya mafunzo ya kibiblia na mazungumzo ya kindugu .Baba Mtakatifu anasema,kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwapo na fursa ya kukaribiana katika mazungumzo yenye manufaa na kuzaa matunda: halikadhalika, kumekuwa na utambuzi na ujuzi wa kina kwa pamoja na katika kuimarisha uhusiano na urafiki.

Azimio la hati ya Yerusalemu na Roma haifichi, hata hivyo, tofauti za kiteolojia za mila zetu za imani;Kwasababu inaonesha ushirikiano wa  karibu zaidi leo na baadaye. Baba Mtakatifu anasema Hati hiyo nawalenga zaidi wakatoliki na kuwapa wito wa kuwa washiriki wa karibu na marafiki na ndugu katika kutafuta kwa pamoja ulimwengu ulio bora ambao unaweza kufurahia amani , haki ya jamii na usalama.

Hatua nyingine inatambua kuwa licha ya tofauti za kina zilizopo za  kiteolojia baina ya Wakatoliki na Wayahudi  ni kwamba wanashirikisha imani ya pamoja na hivyo  dini lazima ziwe na tabia ya maadili na elimu ya dini, na wala siyo vita,au kulazimisha au shinikizo bali kuzidi kuhamasiha jambo ambalo ni muhimu sana . Bwana awabariki na kuangaza ushirikiano wetu ili tuwe pamoja kuweze kupokea na kutekeleza mipango iliyo bora zaidi, mipango ya amani na siyo ya majanga, kwa ajili ya maisha endelevu ya tumaini" (Ger 29:11).

Katika fursa ya ziara yao Baba Mtakatifu ameonesha utashi wake wa kuwatakia  heri ya sikukuu njema ya mwaka mpya wa Kiyahudi  ambao utaanza kwa wiki chache zijazo na hivyo ametamka maneno ya kiyahudi haya  Shanah towah! (Heri na mwaka mpya. Amemalizia na shukrani zake tena na kuwaomba wamkubuke katika sala zao.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.