2017-08-30 14:31:00

Kard. Zenari:Hali ya kivita nchini Siria bado ni mgogoro mkubwa


Ishara za matumaini zipo japokuwa bado kuna ugumu wa kupata suluhisho. Tangu mwanzo wa mwaka huu watu wameanza kurudi  katika vijiji vyao ambao ni karibia watu 600,000 waliokuwa wamekimbilia nchi za jirani, lakini wakati huo bado kuna wimbi la wakimbizi 800,000 waliosongamana kwa namna hiyo idadi hiyo inatia huzuni.Ni maelezo ya  Balozi wa Kitume wa Vatican nchini Siria Kardinali Mario Zenari, katika mahojiano na Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia akiwa anashiriki naye  kutoa hotuba yake katika Mkutano unaoendelea huko Rimini. Huo ni Mkutano wa urafiki kati ya watu nchini Italia uliofunguliwa tarehe 20 Agosti 2017 na ambao unafanyika kila mwaka huko Rimini nchini Italia ukiwa umefikia toleo la mwaka wa XXXVIII  katika lengo la  kutafakari kwa kina mambo msingi ya kijamii kwa ujmla  ili kuhamasisha na kukuza maisha ya watu ya kila siku kwa njia ya kujikita kwa kina kutazama mambo ambayo yanapitia katika mtazamo  lakini wengi hawana utambuzi wa kina wa hali halisi.

Kardinali  Zenari ameeleza hata kuanzishwa kwa hostpitali ambayo iko wazi kwa ajili kuwasadia wenye shida. Akikimbuka mwaka wa huruma, naye ameweza kuwatembelea wagonjwa na kuona majanga ya Siria  hasa kutazama Hospitali nyingi na vituo vya afya vilivyo haribika kutokana na mapigano ya kivita nchini Siria. Hata hospitali tatu Katoliki haziwezi kufanya kazi ipasavyo kwani zinahitaji ukarabati wakati huo  gharama ni kubwa kupindukia. Watu hawana kazi kwa njia hiyo hawana hata bima ya afya ili kuweza kwenda kupata matibabu.
Katika maelezo yake, anaonesha jinsi gani roho yake ilimuuma kuona wadi nyingi zimefungwa, maana vituo hivyo ni nusu magofu, iwapo mwanzo hospitali hizo zilikuwa zikifanya kazi asilimia mia moja ya watu lakini leo hii ni taabu tu. Kuona hivyo ndiyo wazo likamjia la  kufungua Hospitali Katoliki kwa ajili ya maskini wote bila kujali dini na kabila.

Kardinali Mario Zenali ni Balozi wa Vatican nchini Siria tangu mwaka 2008, alikwenda huko kabla ya kuanza vita vya umwagaji wa damu. 2013 bomu lililipua nyumba yake na kuharibu kila kitu, lakini kwa bahati nzuri alinusurika maana  alikuwa ametoka muda kitambo katika nyumba hiyo. Ameishi kwa mateso katika nafsi yake akishiriki mahangaiko ya nchi ya Siria na watu wake. Aidha yeye mwenyewe anatoa ushuhuda kuwa mateso yanafanana kwa kila mmoja. 

Kuhusiana na mtazamo  wa wakristo  kurudi katika nchi yao hasa wale walio lazimika kikimbia magaidi wa serikali ya kiislam huko Siria, Kardinali anasema vita siyo kufikiri  vimekwisha, bali vitadumu bado miezi na miezi. Wale waliokimbilia Ulaya hawatarudi tena kwa sasa. Lakini watu wa kwanza walio rudi kutoka Lebanon na kurudi katika vijiji vyao ni kwasababu vita imepunguza nguvu zake na ndiyo maana wameamua kurudi katika vijumba vyaojapokuwa ni  nusu magofu. Lakini inabidi kutazama mahitaji ya watu hawa 600 waliorudi, na wengine 800 elfu ambao wameacha  mji kama wa Ragga ambapo bado kuna mapigano, hivyo hao ni wakimbzi ndani ya nchi yao; Kardinali Zenari amemaliza, kwa maelezo hayo ni kuonesha kuwa vita nchini Siria ni kipeo kikubwa sana.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.