Yapo mashtaka kuhusu kikosi cha wanajeshi wa kulinda usalama cha Umoja wa Mataifa katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwamba hawalindi raia kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha katika vijiji vya kusini mashariki.Wamekuwapo kwa ajili ya kulinda amani lakini badala yake wameacha mji na kuondoka. Huu ni ujumbe wa Padre Jean-Alain Zembi , paroko wa Kanisa la Mtakatifu Yohane mbatizaji huko Zemo, Parokia iliyoko mpakani na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akielezea jinsi gani Kikosi cha kulinda usalama cha Umoja wa Mataifa hawajali watu na kwamba wanahusika na watu waokufa pia wale wanaojiandaa kufa kutokana na ukosefu wa ulinzi.
Ujumbe ulio tolewa mapema mwezi huu,Padre amesema karibia wazalendo 30 wameuwawa
na vikundi vya wanamgambo wenye silaha waliposhsmbulia kituo cha polisi na hopitali
na nyumba nyingi kuchomwa moto na kuiba vitu vyenye thamani. Wanajeshi wa Kikosi cha
Umoja wa Mataifa kutoka nchi ya Morocco mwanzo wali weza kuwalinda raia mahalia, lakini
hawakuweza kuwalinda na kuwatete watoto na wanawake wasio kuwa na hatia anathibitisha.
Hata hivyo wanajeshi wa kikosi cha Ulinzi wa Umoja wa Mtaifa kutoka nchi ya Morocco
wamefunguliwa mashtaka na siyo tu kukosa kulinda raia, bali hata kuwaua rai wasio
kuwa na hatia. Vilevile Imam Oumar Kobine Layama, kiongozi wa Umoja wa madhehebu ya
Kidini nchi ya Jumhuri ya Afrika ya Kati hivi karibuni alikuwa ameomba waondoke
katika eneo hilo mwaka huu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |