2017-08-28 15:22:00

Afrika ya Kusini: Utume wa Kifranciskan wa Wakatekumeni wapya


Kuanzia tarehe 11 hadi 21 Agosti wanaume na wanawake 72 wa Chama cha Kitume cha Wakatekumeni wapya nchini Afrika ya Kusini, katika kujibu wito wa Baba Mtakatifu Francisko wametumwa katika utume wawili wawili , wakiwa na Biblia mikononi kwa ajili ya kutangaza Habari njema nchini Afrika ya Kusini, Swaziland, Botswana na Lesotho. Aliye wabariki katika kuanza utume huo ni Askofu Mkuu wa Jimbo la  Cape Askofu Brislin ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kusini mwa Afrika(SACBC), na wakati wa maadhimisho ya misa alirudia maneno haya “ kwa njia ya ubatizo tunashiriki kama mitume kwenye huduma ya Yesu Kristo katika kutangaza Ufalme wa mbingu.Uinjilishaji katika nyakati za kisasa , siyo tu kupeleka Yesu kwa wale ambao hawajawahi kusikia juu ya  Yesu, bali hata kwa wale ambao kwa nyakati za sasa Yesu siyo muhimu kwao il kuweza kuwasha imani yao kwa upya.

Utume huo upo kwa sasa katika mchakato wa dunia nzima, kama vile Baba Mtakatifu Francisko alivyowatangazia Vijana zaidi ya 150,000 Chama cha Kitume cha Wakatekumeni wapya walio kuwa wameudhuria  Siku ya Vijana Duniani  huko Poland wakiwa katika mkutano wao kuhusu wito.
Utume huu siyo kwa  watu tu walio wekwa wakfu, hayo ni maneno ya Msimamizi wa  wa chama cha Kitume cha Wakatekumeni wapya  Kusini mwa Afrika, Padri Dino Furgione, kwa maana ya kwamba utume huo umefanywa na wana ndoa, wasio kuwa na ndoa, vijana, wazee, mapadre na waseminari. Hiyo ndiyo moyo wa Baraza Kuu la Mtaguso Mkuu  wa II wa Vatican, ni mwili wa Kanisa na  kama uwepo halisi wa Kristo.

Aidha anaongeza kusema, wamefanya uzoefu ya kwamba Kristo mwenyewe anawasindikiza. Kwa kujibu swali ambalo anaweza kuuliza kama isemavyo Injili ya Luca; Je nilipokutuma kwenda nje bila mfuko wala viatu, je ulikosa kitu chochote? Tunaweza kutoa ushuhuda kwamba hatujakosa kitu chochote kile pamoja na kwamba  wengine ndiyo wameteseka kwa ajili  ukosefu wa mambo fulani lakini pia wamefanya uzoefu wa furaha kamili kama ile ya Mtakatifu Francisko wa Asizi,kwani hata yeye alitumia njia hiyo ya kuwatuma ndugu wadogo wawili wawili.

Sr Angela rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.