2017-08-24 17:40:00

Ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya Video kwa wanachuo Argentina


Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe kwa njia ya Video katika  chuo Kikuu cha wanafunzi wa magereza  cha Ezeiza nchini  (Argentina. Katika ujumbe huo kwa njia ya video anawatumia salam kama alivyozea kuwatumia  kwa njia ya simu wafungwa wa magereza kila Jumapili. Anasema kuwa anazo habari zote kuhusu shughuli zao za chuo wanazofanya kwa njia hiyo ni furaha yake kuona wanapata fursa ya kushiriki katika kazi, shughuli za kiutamaduni na maendeleo, na kuwa hizo ni ishara ya ubinadamu.

Isingewezekana kama isikuwapo watu wenye ubinadamu  kati  yaani viongozi wa ndani ambao  wakala wa huduma ya magereza,wakurugenzi, majaji, wanachama wa Chuo Kikuu cha Buenos Aires na wanafunzi. Ametaja jinsi walivyotoa msukumo wa ufunguzi wa kozi ya muziki , akiwashukuru wote walio shirikiana katika juhudi hizo, kama vile Mkuu wa Magereza, Mkurugenzi, misaada ya  mapendekezo  kutoka Chuo Kikuu cha Buenos Aires na madaraka ya mahakama hasa Makatibu wakuu wa mahakama Kuu na wote walioshiriki katika kituo hicho cha wanafunzi walioko magereza.

Baba Mtakatifu anasema; ni pumzi ya uhai anayoendelea ndani ya  adhabu kati yenu. Na maisha kama mjuavyo ni zawadi lakini zawadi hiyo lazima kuishindania kila siku. Tunaipokea zawadi hiyo lakini tunahitaji kushindana kila siku na lazima kuishindania kwa kila hatua ya maisha yetu; japokuwa ni zawadi isiyokuwa rahisi kuitunza. Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anawatakia wawe wajasiri kila siku kwa maana, matatizo ni mengi na kila mmoja anayo matatizo; lakini tunao wajibu wa kutunza zawadi na kuifanya ikue na katika kutambua hilo,  basi ipate kunawiri.

Kuwa ndani ya magereza ni kutumikia adhabu,ni adhabu kwa ajili ya makosa yaliotendeka. Lakini msisahahu kuwa ili adhabau iweze kuleta matunda ni lazima kuwa na upeo wa macho ya matumaini la sivyo ni kubaki umejifunga mwenyewe na ikawa ndiyo zana ya mateso, isiyo toa matunda. Kutumikia adhabu ukiwa na matumaini ndiyo matunda. Ni matumaini ya kuunganishwa na jamii, kwa njia hiyo malezi ya kijamii, kutazama wakati endelevu ndiyo njia mnayopaswa kutazamia. Katika kozi mpya ya muziki ni kutazama namna ya kuingia kwa upya katika jamii , maana tayari ni kuanza kujiingiza upya kwa njia ya masomo, katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires. Baba Mtakatifu  anarudia kuwatia moyo ya kwamba matatizo hayakosekani, lakini upeo ni mkubwa zaidi ya matatizo na matumaini yanashinda matatizo yote.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.