2017-08-23 15:15:00

Papa:Fikirieni mateso ya watoto, vilio vya akina mama na wakimbizi


Tumemaliza kusikiliza Neno la Mungu kutoka katika Kitabu cha ufunuo kwamba; Tazama nafanya yote mapya.Tumaini la mkristo  msingi wake ni imani kwa Mungu ambaye daima anafanya mpya katika maisha ya binadmu, anafanya mapya katika historia na kufanya mapya katika ulimwengu. Mungu wetu ni Mungu anayefanya mapya kwasababu ni Mungu wa mshangao. Kwa njia hiyo ni wa habari na mshangao.Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo wakati wa kufanya  tafakari ya Katekesi  Jumatano tarehe 23 Agosti kwenye ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI. Baba Mtakatifu ameanza na tafakari hiyo akiongozwa na somo la Ufunuo kwa siku hii ikiwa ni katika mwendelezo wa matumaini ya Mkristo.

Siyo ukristo kutembea ukiwa unatazama chini kama watembeavyo nguruwe, maana daima wanatembea hivyo  bila kutazama juu zaidi ya upeo. Utafikiri kwamba maisha yetu yanazimika hapo katika  kilometa chache  za safari yetu;  kana kwamba maisha yetu hayana lengo na hakuna nafasi ya kukaa; kana kwamba sisi tunalazimishwa kuzurura daima bila sababu yoyote katika magumu yetu yote. Baba Mtakatifu anasisistiza hiyo siyo njia ya mkristo. 
Katika sura ya mwisho wa kitabu cha Ufunuo, zinaonesha upeo wa mwisho wa safari ya mwamini ambayo ni kuelekea katika mji mpya Mtakatifu Yerusalem. Yohane anao mtazamo wa kuona hema kubwa sana ambamo Mungu anawapokea watu wote ili waweze kukaa naye daima (Uf 21,3).

Je Mungu atafanya nini hatimaye tukiwa naye? Atakuwa na huruma yake isiyo na kifani kwa ajili yetu; kama baba anaye pokea wanae ambao wamechoka na mateso mengi. Mtakatifu  Yohane anatabiri : Ndipo nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha ufalme ikisema: “Tazama! Hema la Mungu liko pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena. Mambo ya zamani yamepitilia mbali.” Na Yule aliyeketi juu ya kiti cha ufalme akasema: “Tazama! Ninafanya vitu vyote kuwa vipya.

Baba Mtakatifu anaendelea;jaribuni kutafakari katika maneno matakatifu, siyo kufanya mchezo,bali baada ya kuona matukio ya nyakati zetu katika luninga na magazeti, mahali ambapo zinasikika habari za kutia huzuni na masikitiko ambapo zinatualika kuwa makini. Kutokana na habari hizo za kusikitisha,Baba Mtakatifu Francisko anasema amewasalimia watu kutoka Barcellona; ni habari ngapi zenye kutia huzuni kutoka huko, baadhi kutoka Congo na habari nyingine nyingi, kati ya hizi za nchi mbili zilizotajwa. Jaribuni kufikiria watoto wangapi  wenye woga wa vita, machozi ya mama wengi, ndoto za vijana wengi, wakimbizi wanaokabiliana na safari ngumu, wakati huo manyanyaso na dhuluma wanazozipata …kwa hakika katika hali hii inakujia mawazo na kusema kuwa maisha ndiyo hayo, labda.Lakini pamoja na hayo  yupo  Baba anayelia machozi ya huruma kwa ajili ya watoto wake. Baba nayesubiri kuwambembeleza kwasababu anatambua mateso makao yao ya wakati ujao tofauti na hayo wanayoyaishi. Na ndiyo upeo wa matumaini ya kikristo unaojipanua kila siku katika maisha  ili kuzidi  kutuinua.

Mungu hakukosea kuumba maisha yetu au kujilazimisha yeye binafsi kumwacha binadamu katika usiku wa mgumu na mateso. Mungu ametuumba tuwe wenye furaha. Ni Baba yetu na sisi leo hii tuko hapa muda huu, kufanya uzoefu wa maisha ambayo siyo yale aliyoyataka mwenyewe. Yesu anatoa uhakika kwamba Mungu mwenyewe anatenda kwa ajili ya ukombozi wetu.Tunatambua ya kwamba kifo na chuki siyo mambo ya mwisho kutamkwa katika maisha ya mwanadamu. Kuwa mkristo maana yake ni kuwa na mwelekeo yaani mtazamo wa matumaini. Wengine wanaamini kwamba maisha yanatunza  furaha zote za ujana na za wakati uliopita na kwamba kuishi ni kipindi kinachoisha polepole. Na wengine wanaamini kwamba furaha yetu ni matukio ya muda mfupi na maisha ya binadamu yameandikwa ubatili mtupu. Wengine mbele ya majanga mengi husema maisha hayana maana.

Njia yetu ni ile isiyo kuwa  maana. Lakini kwa upande wa Wakristo hatuamini hivyo. Imani yetu  ni kwamba katika upeo wa binadamu kuna jua linalo angaza daima. Tunaamini kwamba siku nzuri zaidi ziko mbele zinakuja. Sisi ni zaidi ya kipindi cha kiangazi na Vuli. Anaongeza kutoa mfano wake binafsi ya kuwa yeye anapendelea kuuliza swali na kila mmoja ajibu kwa nafasi yake katika moyo wake kwa kimya, je mimi ni mwanaume, mwanamkeì, kijana , wa kiangazi wa vuli? Moyo wangu ni wa kiangazi au wa vuli.?

Kila mmoja ajibu, kama anajitambua kuwa mbegu ichanuayo katika dunia mpya badala ya majani ya njano katika matawi. Tunajidanganya, tuna majuto na maombolezo; tunatambua kuwa Mungu anataka sisi kuwa warithi wa ahadi bila kuchoka kupalilia ndoto. Baba Mtakatifu anasisitiza ya kutokusahau swali hilo kama wewe ni mtu wa kiangazi au wa vuli. Kwa maana ya  Kiangazi anayesubiri mau , anayesubiri matunda , anayesubiri jua ambalo ni Yesu au wa vuli anayesubiri akiwa daima amelekeza uso wake chini  kwa uchungu; kama wakati mwingine nilivyokwisha sema ukiwa na sura ya pilipli au ya siki, Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa  hapana isiwe hivyo. 

Mkristo anatambua kuwa Ufalme wa Mungu na Ukuu wa upendo unakua kama shamba kubwa la ngano hata mbele ya magugu mabaya. Daima kuna matatizo, kuna masengenyo, kuna vita na magonjwa. Lakini ngano inazidi kukua na mwisho ubaya utaondolewa. Hatujuhi  wakati ujao lakini tunatambua kuwa Yesu ni neema kubwa ya maisha, ni mkono wa Mungu anaye tusubiri siku ya mwisho kutukumbatia, lakini hata leo hii anatusindikiza na kututuliza katika safari yetu. Yeye anatusindikiza kutufukisha katika hema kubwa la Mungu tukiwa watu wengi  (Uf 21,3), ndugu, kaka na dada, tutampelekea kumbukumbu za siku tulizoishi hapa duniani. Itakuwa vizuri zaidi kugundua kuwa hatukuweza kuteseka bure,hakuna vicheko na machozi vitakavyopotea. Hata katika maisha ambayo utafikiri yamekuwa marefu, wakati huo huo yataonekana na upulizo.

Katika kitabu cha Mwanzo,kazi ya uumbaji haiishi katika siku ya sita bali  inaendelea bila kuchoka kwakuwa Mungu daima amekuwa akihangaikia sisi. Hadi mwisho wa siku ile itakapo fika,siku ile ya asubuhi ambayo haitakuwa na machozi, utuakuwa ni muda huo ambao Mungu anatatamka maneno ya mwisho ya baraka akisema:Tazama! anasema Bwana,nafanya mapya.Baba yetu ambaye ni Mungu wa habari mpya, ni Mungu wa mshangao. Siku ile sisi tutakuwa na furaha ya kweli?. Ndiyo tutalia kwa machozi lakini ya furaha; Baba Mtakatifu Francisko amemalizia katekesi yake ya siku ya leo.

Mara baada ya katekesi yake ametoa salamu nyingi kwa mahujaji wote waliofika katika Ukumbi wa Mwenye heri Papa Paulo VI kusikiliza katekesi hiyo. Na mwisho wa sala amemalizia na maneno ya faraja na uwepo wake karibu wa sala kwa watu wote wanaoteseka kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea Jumatatu 21 Agosti katika Kisiwa kimoja cha Ischia nchini Italia na kusababisha majeruhi wengi na nyumba nyingi kuharibika . Baba Mtakatifu Francisko anawaombea walio kufa na majeuruhi wote, aidha familia wote walio poteza nyumba na mali zao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.