2017-08-23 16:07:00

Mazishi ya Balozi wa Kitume Mario Roberto Cassari huko Sardegna


Mkarimu na mwenye kujituma katika kusikiliza Injili kwa upendo na mapapa. Amefanya utume wake nje na ndani ya nchi  katika kwa niaba ya huduma ya Vatican. Ni maneno ya Askofu Mkuu Angelo Becciu ambaye ni  Katibu Mkuu msaidizi wa Vatican wakati wa Ibada ya Misa takatifu kwa ajili ya Kumwombea Balozi wa Kitume Mario Roberto Cassari aliyeaga dunia tarehe 19 Agosti 2017, na mazishi yake yalifanyika tarehe 21 huko Ghilarza kisiswani Sardegna nchini Italia alikozaliwa. Ibada ya misa iliudhuliwa na maaskofu wa Sardegna na idadi kubwa ya mapadre, watawa,wakiwemo viongozi wa serikali, wanajeshi na waamini wengi katika parokia.

Katika Mahubiri yake, Askofu Mkuu Becciu ameleezea hatua mbalimbali na muhimu za huduma yake aliyofanya wakati anaishi. Amemkubuka ni jinsi gani Balozi Cassari alikuwa anatambua utashi wa Bwana na fursa zake  za kuwa mkarimu katika huduma ya Kanisa na ya Baba Mtakatifu kila mahali popote alipotumwa.Marehemu Balozi Mario Roberto Cassari daima alipotumwa katika nchi zozote alifanya huduma hiyo kwa hekima na bidii  na kuwa na dhamiri nyoofu katika njia ya Jumuiya  katoliki katika upeo  wa ushirikiano na Vatican.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.