2017-08-22 12:21:00

Papa ametuma barua ya matashi mema ya Sinodi ya makanisa ya Wametodisti na Wavaldese


Kuanzia tarehe 20 hadi 25 Agosti nchini Italia Makanisa ya Wametodisti na Wavaldese wanafanya Sinodi yao ya Mwaka. Wawakilishi ni 180 wakiwemo wachungaji na walei ambao wameungana kwa pamoja kutafakari mada nyingi  kama vile : kuanzia miaka 500 ya mageuzi ya kianglikani, suala la wahamiaji, mapokezi na  kushirikisha; mazungumzo ya kiekumene na katika shughuli za kijamii kujihusisha na wahitaji,vilevile mada nyeti inayohusiana na mwisho wa maisha ya mtu, changamoto za kuhubiri katika ulimwengu ambao unazidi kuwa na migogoro, halikadhalika kujadili juu ya lugha na misemo mibaya inayojitokeza katika nyakati hizi,utofauti kati ya watu unaojitokeza, aidha kuhusu familia na mitaji  bila kusahahu mahusiano ya kimataifa ambayo makanisa ya Wametodisti na Wavaldese wanajikita kwa ndani zaidi.

Katika tukio la Sinodi ya ya mwaka naye Baba Mtakatifu Francisko amewatumia barua ya kuwawatikia matashi mema kwamba,  katika fursa ya ufunguzi wa Sinodi hiyo anaonesha ukaribu wake kwa niaba ya Kanisa Katoliki. Anatoa salam zake za kindugu kwa kuwahakikishia ukaribu wake wa sala. Aidha anasema bado anazo kumbukumbu za mkutano wao wa hivi karibuni huko Torino na Roma, kama vile wa huko Argentina. Anawapongeza kwa ajili ya ushuhuda wao alioupokea na sura nyingi ambazo siyo rahisi kwake kusahau. Matashi mema yanawandea kwa dhati wanaposhiriki katika tafakari ikiwa ni sambamba na  maadhimisho ya miaka 500 ya mageuzi ya Kanisa la Kianglikani.Anasema Baba Mtakatifu kuwa, waongozwe na furaha mbele ya uso wa Yesu, kwani uso wake unao watazama ni chemi chemi ya  amani yetu,Yeye anafanya tujisikie kuwa wana wapendwa na Baba, anafanya tuone wengine, dunia na historia kwa mtazamo mpya.

Anaendelea Baba Mtakatifu,mtazamo wa Yesu uangaze mahusiano tuliyo nayo, kwasababu yasiwe tu rasmi na sahihi, lakini pia yawe ya  kindugu na hai. Kuwa mchungaji mwema inahitaji kutembea kwa pamoja na mtazamo ambao tayari unawakumbatia wote yaani mitume wake ambao anataka kuwaona katika umoja. Kutembea katika mwelekeo wa umoja na katika mtazamo wa matumaini yanayo tambua uwepo  wa Mungu mwenye nguvu zaidi kuliko mabaya ni muhimu. Hiyo hasa zaidi leo hii katika ulimwengu wenye ishara za vurugu na hofu, dunia iliyo jaa majeraha pamoja na utofauti, mahali ambapo ubinafsi wa kujinufaisha kwa gharama za wengine unaficha uzuri wa kupokeana, kushirikishana na kupenda. Lakini ushuhuda wa kikristo hauwezi kamwe kuangukia katika mantiki za dunia hii, kwa njia hiyo kwa pamoja hebu kusaidiana kuchagua kuishi mantiki ya Kristo.  Amemalizia barua yake akiwashukuru na kuwaomba wasisahau  kusali kwa ajili yake na kwa ndugu na kaka.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.