2017-08-21 16:00:00

Wiki ya Liturujia mjini Roma: Liturujia hai katika Kanisa hai


Jumatatu  21 Agosti 2017 umefunguliwa Mkutano wa 68 Wa Wiki ya Liturujia Kitaifa mjini Roma ikiwa na “kauli mbiu Liturujia hai kwa ajili ya Kanisa hai”.Ni tukio lnaloandaliwa kila mwaka na Kituo cha utendaji kitaifa cha Liturujia nchini Italia. Chama hiki kilizaliwa Oktoba 1947 ambacho kimetoa mchango mkubwa katika maandalizi ya ardhi ya Mkutano wa Mtaguso wa pili wa Vatican kwa namna ya pekee katika wiki ya Liturujia kitaifa. Mkutano wa wiki ya Liturujia ulio funguliwa 21 Hadi 24 Agosto mjini Roma ni fursa ya kurudia upya katika kujikitaka kwenye  shughuli za Kanisa la mapatano na kuweka mkazo kwamba liturujia ni kiini cha maisha ya imani ya kila mbatizwa.

Askofu Claudio Mangaio wa Jimbo la Castellaneta na Rais wa Kituo cha Liturujia nchini Italia, akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusu kauli mbiu yenye maneno ya kujirudia ya “Liturujia hai katika Kanisa hai”  pia maana ya chama hiki kwa ujumla amesema,  ina maana ya kutaka kuonesha msingi wa liturujia kama mabadiliko yanayo tokana na Mtaguso Mkuu wa  II wa Vatican, zaidi ni kuonesha nguvu ya kuadhimisha liturujia kwamba ni Jumuiya ya kikristo ambayo ina uwezo wa kuchota kutoka chemi chemi hai ya neema ya maisha ya Kanisa linaoongozwa  na kusimamia na  ishara hai. Ishara hizi hai ni maneno na matendo ambayo yana uweze wa kufikia hatma kila mwaamini ambaye pamoja na matendo hayo na kukabiliana  na matatizo yake ya kila siku.
Halikadhalika, liturujia inasaidia katika kipimo cha hali ya juu ya maisha ya utakatifu. Wakati huo huo ni kutaka kuelezea ulazima wa kutokupuuzia kwamba, kutokuelewa vema namna ya kuadhimisha liturujia yaweza kusababisha kutokuzaa matunda mema ya kikristo. Askofu ametoa mfano wa ukosefu wa matunda mema akisema, kwa mfano kuadhimisha liturujia kwa namna ya uchovu bila furaha hiyo siyo  hali ya kuzaa matunda  katika Kanisa linaloitwa kutoka nje.

Katika  kuelezea waraka wa Injili ya furaha  inayotaka Liturujia itoke  nje ni sawa na kutoa mawasiliano kwa maana ya kwamba, kuzungumzia  liturujia ni kuwasiliana daima kwasababu ndicho kitendo cha kuadhimisha na  ambacho ni mawasiliano.Ni  msingi wa habari njema kati ya Mungu ambaye anazungumza na watu wake wanao sikiliza, wanaojitoa sadaka, wanao sifu na kuomba msaada. Liturujia shirikishi matokeo yake ni muhimu ambayo ni mawasiliano ya kidugu na kimisionari kwa maana ya  kutoa maisha ya Kanisa linalotoka nje.  Pasaka inayoadhimishwa kila mwaka kama tendo la liturujia , daima ni mawasialiano ya maisha mapya, ambayo yanawaalika waamini hao wawe na maisha mapya.Hiyo ni kwasababu ni Mungu mwenye huruma ambaye katika Liturujia anatenda kazi yake; kwa namna hiyo hata Kanisa kwa unyenyekevu linatoka nje kwa makini, kwa upendo kuelekea katika ulimwengu mzima ili kutangaza neno jema.

Kwa safari hiyo miaka 70 ya Kituo cha utendaji wa kiliturujia , ni tunda la chama cha kiliturujia, ambacho kwa namna ya pekee kipo nchini Italia na kinajikita kwa undani zaidi katika maisha ya Kanisa la Italia. Kituo hicho kiliandaa ardhi ya mabadiliko ya mtaguso kwa namna ya pekee kwa njia ya maandalizi ya wiki ya liturujia kitaifa . Kituo hiki kiliongoza hatua kwa hatua hadi kufikia mabadiliko ya  kutangazwa katika tamaduni mbalimbali kwa kutoa misingi ya kihistoria , kiteolojia na kiliturujia. Ni mabidiliko ya mtaguso na kutoa matunda yake ya kichungaji.

Kwa miaka 70 ya kuanzishwa kwake, wakati huo huo wiki ya liturujia inafikia  mkutano wa mwaka wa 68 ni kutaka kuonesha kwa upya uraia na utume wake tangu mwanzo na endelevu katika mabadiliko yake mapya ya kujikita katika shughuli ya huduma ya Kanisa la mapatano.
Hali kadhalika ni kwa namna ya pekee  kuwa na mtamzamo wa  kutaka kuzuia kwamba maisha ya Kanisa yasiwe kito tu cha sanaa au kujibinafsisha kwa walio wachache. Hiyo ni Liturujia hai kwa Kanisa hai lenye uwezo wa kusema na kutangaza wajibu wa Mungu kwa binadamu wa leo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.