Mawasiliano katika mtazamo wa Baba Mtakatifu Francisko, ndiyo ilikuwa kichwa cha hotuba ya Mosinyo Dario Vigano Rais wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican (SpC) wakati wa kufungua Mkutano wa 10 wa Mawasiliano ulio andaliwa na Baraza la Maaskofu nchini Brazili. Mkutano huo umefunguliwa tarehe 16 Agosti na utamalizika 20 Agosti.Mbele ya umati mkubwa wa waandishi wa habari na wahudumu wa mawasiliano huko Jimbo la Joinville Mkoa wa Mtakatifu Catarina Brazil; ametoa hotuba yake, ikiwa imegawanyika katika sehemu mbili, ambapo sehemu ya kwanza ikioonesha juu ya mawasiliano ya Baba Mtakatifu Francisko. Amesema kwamba kabla ya kujikita kwa kina juu ya mageuzi, ni lazima kutambua mtazamo wa hali ya halisi ya mawasiliano ya Baba Mtakatifu Francisko, ni mawasiliano ambayo yaweza kuelezwa kuwa kwa namna ya kisayansi. Na zaidi amesema, katika matukio mengine anapenda kusisitiza ni jinsi gani Baba Mtakatifu Francisko alivyo na uweza wa kuunda misemo ambayo ni kama aina ya mawasiliano, kwa kutumia ubunifu na urahisi usio wa kawaida, au kwa kutumia mifano na mafumbo.
Monsinyo Vigano’ amekazia kwamba, hiyo ni namna yake ya kuwasiliana na kila mmoja,ili
kupunguza pengo kubwa linaloweza kujitokeza kuwezesha mwendelezo wake wa mazungumzo
wakati wa kuwasiliana
Aidha amesema ni kwa njia ya maelezo na yenye kuwa na huruma ambavyo ni msingi mkubwa
wa Baba Mtakatifu wakati wa mawasiliano yake. Mawasiliano hayo siyo kwamba yanatoka
nje tu badala yake ni nyenye thamani ya kukuza uwepo wake na mahitaji wa wasikilizaji
wake pia. Lugha anayo tumia Baba Mtakatifu Francisko haisimami kamwe na wala kuwa
nzito au kuchosha msikilizaji zaidi ina uwezo daima wa kuvutia na kuisikiliza sauti
yake. Ametoa mfano kuwa, tendo la kusikiliza kwa kawaida ni jambo gumu na changamoto
kwani mara nyingi linakutaka uwe na uhusiano na wengine katika kuwasiliana.
Katika sehemu yake ya pili ya hotuba, Monsinyo Vigano’ amelezeza kwa kirefu na
kushirikisha mchakato wa mageuzi ya Habari Vatican. Ameelezea mwanzo na maendeleo
ya mageuzi ya Mawasiliano hayo ya kwamba yana mzizi mkuu unaotoka mbali na zaidi
sasa kwasababu ya ulazima na dharura ambayo tayari ilianzia katika Jubileo ya mwaka
2000. Mageuzi hayo yameendelea, hadi kufikia hatua ya kiteknolojia ya digitali ambayo
yamebadili namna ya utendaji kwa kila aina ya maisha yetu ya kila siku, ya kijamii,
kisiasa na dini.
Halikadhalika amesema,mageuzi siyo kitu rahisi kama uchoraji kwa kukumbusha maneno
ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoyasema wakati wa Mkutano wao wa mwaka wa Sekretarieti
ya Mawasiliano kuwa; Mageuzi siyo kupaka rangi vitu kidogo, bali mageuzi ni kutoa
mfano muundo mwingine wa vitu, kuvipanga kwa namna nyingine. Hii ina maana, siyo
kwamba ni utaratibu rahisi tu , lakini pia ni namna ya kujua kubuni mbinu ya kweli
na mikakati ya utoaji wa mawasiliano ya Vatican.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |