Miaka sabini iliyopita, nchi ya Pakistani na India tarehe 14 na 15 Agosti 1947 walitangaza uhuru wao kutoka mikononi mwa Ukoloni wa Kingreza. Lakini matukio ya kihistoria na kisiasa yalizidi kuendelea na mzozo kati ya nchi hizi mbili, matatizo hayo kwanza kabisa yalisababishwa na mvutano wa kanda ya Kashmir. Ki ukweli hali hiyo ya Pakistan na India leo hii iko mbali na Muungano wa taifa kubwa ambao Mahatma Ghandhi angependelea. Kwa mujibu wa Marzia Casolari, profesa wa historia ya nchi za Asia katika Chuo Kikuu cha Turin nchini Italia amesema, sehemu kubwa ya msuguano kati ya India na Pakstan itaweza kutatuliwa iwapo utafanyika mgawanyiko wa sehemu mbili kitaalamu wa Mkoa wa Kashmir wenye kuwa na mgogoro.
Katika maadhimiso ya miaka 70 ya uhuru wa nchi hiyo; hata Kanisa Katoliki limeungana
kwa pomoja katika maadhimisho hayo. Askofu Theodore Mascarenhas, Katibu Mkuu wa Baraza
la Maaskofu Katoliki nchini India ametoa maoni yake akisema; wanashukuru Mungu kwa
nchi hiyo kubwa yenye kuwa na ustaarabu mkuu, kwa ukarimu wao uliyo waweza kupokea
ukatoliki kwa miaka mingi. Askofu anasema, wanafurahi kuwa raia wa India na kuwa na
ustaarabu ambao siku zote umekuwa utamaduni wa kuvumiliana na ushirikiano wa amani
kati ya dini na jumuiya mbalimbali.
Wakiwa wanaadhimisha miaka 70 ya uhuru anaongeza, wanatarajia maendeleo endelevu
katika nchi yao kubwa, hasa nchi ambayo inaweza kutoa kipaumbele kwa maskini, watu
wa kiasili , wadalit na wale waliotengwa.Kwa maana watu hawa wanabaki bado moyo wa
Kanisa , kama Yesu mwenyewe alivyo fundisha.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |