Tume ya Kitaifa ya Haki na amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki wa Pakistani wametoa
wito kwa viongozi wa vyama vya kisiasa kuonesha ukomavu wa kisiasa na kuepuka chochezi.
Wametamka hayo mara baada ya kuondolewa kwa Waziri Mkuu Nawaz Sharif kutokana na
uchunguzi wa kuhusishwa na rushwa. Maaskofu hao wanao wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka
kwa vurugu ambazo zinaathiri wanachi na siyo tu wakristo.
Taarifa inakumbusha kuwa matukio ya kisiasa ambayo makahama Kuu imemwondoa Sharif
tarehe 28 Julai 2017, inazidi kuleta mvutano na vurugu kubwa nchini humo. Kwani inasemekana
watu zaidi ya Ishirini wamejeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa
ndani ya Lori la kubeba matunda tarehe 7 Agosti 2017 huko Lahore. Wakati huo hivi
karibuni katika mji huohuo watu ishirini na sita wakiwemo Wakristo watatu waliuwawa
katika shambulio la kujitoa muhanga.
Hata Kiongozi wa kundi la madhehebu kwa ajili ya amani kiitwacho Rawadari Tehreek
ameonesha wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mivutano hiyo ya kisiasa, anasema kutumia
vibaya utamaduni utaongeza moto zaidi katika jamii ambayo imechoka kuvumilia migogoro
hiyo. Aidha ameongeza, ipo ofu ya kumwaga damu tena katika mwelekeo wa uchaguzi mkuu
uliopangwa kufanyika mwaka kesho. Kwa njia hiyo Kiongozi huyo Samson Salamat ambaye
ni Rais wa Madhebu ya Kikristo amewaalika kupiga marufuku ya kufanya mijadala ya
chuki. Ikumbuke kwamba Katika nchi ya Pakistani Bwana Sharif alikuwa ni waziri Mkuu
wa kumi na tano katika nchi ya Pakistani ambaye hakuweza kukamilisha mkataba wa katiba
ya uongozi kwa miaka mitano.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |