2017-08-14 09:15:00

Patriaki aonesha wasi wasi kwa Wakristo huko Mashariki ya Kati


Tunao wasiwasi mkubwa kwa sababu ya vurugu na vita ambavyo vinazidi kuyumbisha nchi za Mashariki  kwa namna ya pekee Siria, Iraq na Misri, hii ni sauti ya kilio chetu tukipaza sauti zetu katika Jumuiya ya Kiataifa ; fikirieni namna yetu ya kuweza kustahili kuishi. Matumaini na imani ya wakatoliki na wakristo wengine wa Mashariki bado wana nguvu, lakini hofu  kubwa ni ile ya kuona tumesauhulika kama waathirika wachache na vurugu hizi. 
Huu ni ujumbe wa nguvu ambao umesikika katika maneno ya Patriaki wa Antiokia Ignace Joseph II Younan, mwanachama wa Baraza la Kipatriaki Katoliki katika nchi za Mashariki wakati akitoa hotuba yake  wakati wa Mkutano ambao umemamalizika huko Diame nchini Lebanon hivi karibuni. Ni mkutano wa mapatriaki baada ya miaka miwili ya mapumziko kwa sababu ya vita na ukosefu wa usalama. Katika ajenda zao wamekabiliana na  mada muhimu za sasa hasa; hali ngumu ya sasa ya jamii ya Kikristo, nchi ya Siria na  katika sehemu kubwa ya Mashariki ya Kati, uchungaji wa kitume, matatizo na dharura ya kijamii kisiasa.

Patriaki Younan ameeleza kuhusu Jumuiya Katoliki na zaidi namna ya wakristo wanavyoishi, amesema  kwamba ni kama wanaishi katika maandaki. Anatamani kuona mwisho wa vita hivi na vurugu zitokanazo na  vikundi mbalimbali vya kijihadi vyenye silaha. Vile vile namna inavyo jitokeza  unyonyaji  wa kisiasa kwa kujinufaisha katika njia za kimataifa, ambazo wanafikiria nchi za mashariki ni maeneo ya kujinufaisha kiuchumi na kimikakati. Aidha Patriaki Younan anasema wazi kwamba, wakristo wengi wamekimbia na hawatarudi makwao hasa vijana kwasababu wametishiwa imani yao, haki za kibinadamu na uraia. Kama wachungaji anasema, wanajikita zaidi  katika utume wa  kusaidia na kulinda watu. Hiyo ni kutokana na  utambuzi wa hofu nyingi na wasiwasi wa watu wao wali nao. Anathibitisha kuwa wanabaki nao kwa kuwahakikishia uwajibu ma mshikamani wao mahalia na ulimwenguni, aidha kuwatia moyo wote ili waendelee kuwa shuhudia imani na matumaini.

Pamoja na hayo katika mkutano wa mapatriaki , wametazama hali tete ya nchi ya Lebanon, kwa sababu ya kufurika kwa wingi  wakimbizi zaidi wanaotoka nchi ya Siria. Kama ilivyojitokeza wito kwa siku zilizopita hata Patriaki ameonesha wasiwasi huo tenge wa nchi hiyo.  Anasema inahitaji kwa haraka kupata ufumbuzi wa jambo linalowafanya  watu wanakimbia , lakini pia  hata mipango na mikakati ya kimataifa iweze kuwalinda watu wa Lebanon ambao wanasaidia kwa hali zote wakimbizi hadi watakaporudi katika nchi zao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.