2017-08-14 17:01:00

KENYA:Viongozi wa madhehebu ya dini kuomba amani na utulivu wa nchi


Hakuna kufanya vurugu bali kufuata njia ya utulivu ili kuzuia ghasaia; ndiyo ulikuwa wito wa viongozi wa dini mbalimbali za Kenya wakati wa Jukwaa lao wakati wakisubiri matokeo rasmi ya kura za uchaguzi wa Rais nchini Kenya. Hata hivyo baada ya kutangazwa kwa kura hizo za kushinda kwa Rais Uhuru Kenyetta,mpinzani wake Raila Odinga hakukubaliana na matokeo hayo kwa kudai kuwa kura zimeibiwa kwa njia ya mtandao.
Lakini wasimamizi wa  uchunguzi wa Umoja wa nchi za Ulaya walitoa taarifa ya kutokuona hitilafu yoyote ya mtandao wakati wa operesheni hiyo ya kuhesabu kura.

Na Peter Karanja Katibu Mkuu wa Baraza la Umoja wa Makanisa nchini Kenya (NCCK) alikuwa ametoa  kauli ya kwamba wamekuwa makini kuhusiana na suala la wasiwasi wa Bwana Odinga na kwa wagombea wengine. Lakini ni muhimu kutokufanya matendo ya ghasia,vurugu na hata shughuli nyingine zinazoleta uharibifu. Aidha katika Mkutano huo alikuwa amesema kwamba, wanayo matumaini katika shughuli za tume ya uchaguzi, kwa kushirikiana na wadau wa kisiasa kutatua matatizo hayo,la muhimu ni kuacha nchi ya Kenya watu waweze kuishi kwa amani wakati wakisubiri matokeo.Vile vile viongozi wa Maknisa ya Kenya akukuwa ametoa pongezi kwa operesheni ya shughuli za ulinzi katika kuhakikisha usalama kabla na baada ya uchaguzi. Lakini hata hivyo ghasia zimeweza kuonekana katika baadhi ya maeneo tofauti ya vijiji  lakini tofauti ya Mji Mkuu Nairobi ambao inasemekana ulikuwa shwali.

Na taarifa kutoka Umoja wa Mataifa kwa njia ya  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amepongeza watu wa Kenya kwa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa amani. Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wake Guterres amesikia matokeo na hatimaye Uhuru Kenyatta kutangazwa na Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwa rais mteule. Hata hivyo Bwana Guterres ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa wanaopinga matokeo ya uchaguzi kuelekeza malalamiko yao kupitia vyombo vinavyokubalika kisheria.

Amewataka  viongozi wa kisiasa watume ujumbe ulio wazi kwa wafuasi wao ili waweze kujiepusha na vurugu huku akisisitiza umuhimu wa majadiliano katika kuzuia uhasama. Bwana Guterres amesema Umoja wa Mataifa, kwa ushirikiano na Muungano wa Afrika na wadau, unashirikiana na mamlaka za kisiasa na na wadau wake  ili kufanikisha kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi kwa njia fanisi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.