2017-08-14 09:38:00

Ingia Tovuti ya Youthsynod2018.va kwa ajili ya vijana ufunguke!


Katika maandilizi ya sinodi ya  maaskofu kuhusiana na  vijana inazidi kupamba moto .Wakati huo ,Baba Mtakatifu Francisko katika Tweet yake ya Jumamosi 12 Agosti 2017 amewataka vijana wote duniani wasikike sauti yao katika Sinodi  inayowahusu, itakayo fanyika Oktoba 2018. Kuanzishwa kwa progam hiyo ya ujumbe wa Baba Mtakatifu  katika tweet  imepokelewa kwa furaha na Kardinali Lorenzo Baldisseri Katibu  Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu ambaye kwa kipindi hiki pamoja na kuwa ni kiangazi anaendelea kufanya kazi kwa ajili ya umuhimu wa tukio hilo la Kanisa kwa mwaka kesho.
Mwandishi wa Habari wa Radio Vatican, amepata kumuhoji Kardinali Baldisseri kuhusiana na program za Baba Mtakatifu Francisko katika kutoa ujumbe wa tweet kwa vijana kwa njia ya mitandao ya kijamii. Kardinali amesema yeye anaungana naye katika ujumbe ambao mara kwa mara anazidi kuutoa, kwa namna ya pekee hata siku ya tukio la kuadhimisha Siku ya Vijana Kimataifa iliyo andaliwa na Umoja wa Mataifa tarehe 12 Agosti 2017. Aidha amesema, wako wanafanya kazi kwa ajili ya maandalizi ya Sinodi ya 2018 ambapo wameweza pia kutoa  umuhimu  wa kusambaza tukio hilo kwa njia ya  mitandao ya kijamii.

Amesisitiza kuwa ikumbukwe ya kwamba hata Sinodi ya maaskofu imeunda  Tovuti mpya onayoiitwa "youthsynod2018.va”.  Vilevile anasema tweet  ni dhahiri kuwa kichocheo kikubwa , kwasababu ni Baba Mtakatifu  mwenyewa ambaye naongea moja kwa moja na vijana. Ameongeza kusema;wakati wa tukio la mkesha wa wiki ya maandalizi kwa ajili ya Siku ya Vijana Duniani , Baba Mtakafu  Francisko  alisema ni  Sinodi ya vijana maana yake ni Sinodi yao wao wenyewe.Halikadhalika katika mahojiano  ameongelea juu ya maswali yaliyotolewa kwa njia ya mtandao kwa ajili ya vijana ili waweze kutafakari na kujibu. Kardinali Baldisseri anmesema, Baba Mtakatifu anahoja nayo, ni lazima kuandaa Sinodi ya vijana na maandalizi ya tukio hilo yawe ya moja kwa moja na vijana . Hiyo ni kwasababu vijana wenyewe wanalazimika kushiriki kikamilifu katika kuwandaa wenyewe kwa maana ndiyo wahusika wakuu, kwa namna hiyo wawe na fursa ya kupata zana, ili kuweza kutoa hoja, zao ambazo  Mababa wa sinodi waweze kuingia moja kwa moja katika ulimwengu wao iwapo vijana wataweza  kutoa vidokezo muhimu  vinaruhusu zaidi ulimwengu wa maisha yao ya baadaye.

Tovuti ya Sinodi ya maaskofu iliyofunguliwa hivi karibuni ina lengo la  kuwashirikisha kwa mapana Kanisa lote la ulimwenguni,  kwa njia hiyo kila Baraza la maaskofu na taasisi zake za ndani wanaweza hata wao kufungua  tovuti mpya, lakini, muhimu kusambaza program hizo  zikafikia tovuti ya  Sinodi ya maaskofu ili kuhakikisha kwamba unakuwa  mtandao mmoja wa dunia,na kwamba kila tukio linalotokea katika parokia ndogo au kubwa, linaweza kujulikana kwa ngazi ya  kimataifa.Aidha Kardinali Baldisseri anasema ratiba yao kanzia tarehe 11 hadi 15 Septemba wanaanza mkutano mjini Roma wakiwa na wataalamu wa mbalimbali wa utafiti kwaajili ya kufanya uchunguzi wa suala la vijana. Wataalam hao, bila shaka, ni watu ambao wanajua kwa kina zaidi  katika hatua za  kisayansi, kuwa na maoni zaidi kutoka kwa wale wanao wasindikiza  ambao pia ni vijana. Ni lazima kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga jamii, ni lazima kuanza na kijana amemalizia Kardinali Baldisseri Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu. 

Vijana wanajenga amani : ndiyo mada ya Siku ya kimataifa ya vijana duniani 12 Agosti  2017 iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kusisitiza jukumu muhimu  kwa vijana katika katika kuziua migogoro kama mawakala wa mabadiliko, na pia wao ni mchango kwa uendelezaji wa jamii ya umoja , wazi kwa ajili ya haki na maendele endelevu. Mpango wa mwaka huu inalenga katika Programu ya Umoja wa Mataifa kwa  ya Maendeleo Endelevu, katika malengo ya 2030, ambapo kipengele cha 16 kinawakumbusha  ahadi yake ya kujenga jamii ya amani , haki , wazi na umakini wa  kutoa majibu ya dhati katika changamoto za kidunia.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.