2017-08-09 15:19:00

Radio Pacis Uganda ya kusanya habari za wakimbizi wa Sudan Kusini


Radio Pacis kwa ajili ya kutoa sauti kwa wale wasio kuwa na haki, na kwasaidia watu katika nchi  ili kuwawezesha wawe na mazungumzo ya amani. Hiyo ndiyo lengo la Radio ya Pacis , ambayo iko Arua nchini Uganda, Radio hiyo ilianzishwa na Mmsionari wa Komboni Padre Tonino Pasolini ambaye ameishi katika nchi za Afrika zaidi ya miaka 38 hivi.Padre Tonino anasema wako nchini Uganda wakipakana na Nchi ya Kusini mwa Sudan ambapo kuna hali kiukweli ya kutisha kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na ukame. Kila siku karibia watu 4 elfu wanao hama kutoka nchi yao na  kukimbilia maeneo ya majimbo ya Uganda. 

Katika miezi sita ya mwisho, zaidi ya watu 750,000 wamefika Uganda kutokea Nchi ya Sudan ya Kusini, zaidi wamefika bila kuwa na choche kile kutoka majumbani mwao. Wakifika katika makambini wanapewa matumizi muhimu ya kwanza . Lakini wanalazimika kujifunza kula chakula ambacho wanapewa, ambacho siyo rahisi kwao kuzoea. Wanapewa hata jembe kwa ajili ya kulima sehemu ya ardhi ili kuweza kukidhi haja ya kuendelea kuishi.
Asilimia 86 ya wakimbizi wanawakilishwa na watoto na wanawake, jambo hili ni tatizo kubwa, anasema Padre Tonino hasa kwa upande wa elimu. Watoto wote waliokuwa wakisoma shule za msingi na sekondari wanapofika nchini Uganda wanaota ndoto ya kuweza kuendelea kusoma , kupata  elimu nzuri kwa ajili ya misha yao ya baadaye.

Kwa sasa Mashirika yasiyo ya kiserikali yanatafuta namna ya kujenga mashule ili kuweza kuwapa kwa namna moja au nyingine matumaini ya vijana hawa. Hata serikali ya Uganda  imefunguliwa shule ambazo zinaweza kuwapokea hata watoto wahamiaji . Ndiyo siyo kazi rahisi inahitajika fedha nyingi, wakati huo huo hata zinatolewa na wafadhiri wa mashirika ya kibiandamu hazitoshi.Radio Pacis imekuwa ni sauti moja ya kuwanya watu duniani watambua hali halisi ya uchungu ulio katika makambi ya wakimbizi kila siku. Kila baada ya siku 15 Padre na kundi lao wanakwenda kutembelea makambi na kufanya meza ya mduara. Waanakutana zaidi ya watu 100 au 200 wwanao udhuria  meza ya mduara. Padre anasema, wanapenda kusikiliza historia zao na matatizo yao, na jinsi gani walifika ili kuweza kuona namna gani ya kusaidia. Aidha nao wanaweza kuwa wahamasishaji wa amani maana bila amani nchi ya Sudan ya kusini haitakuwa na maisha endelevu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kisahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.