Askofu Mkuu Rino Fisichella Rais wa Baraza la Kipapa la Ushauri na Ujilishaji mpya
atakaye ongoza hija ya mwezi huu huko Fatima nchini Ureno. Tukio la hija hiyo
hilo linategemewa kufanyika Jumamosi ya tarehe 12 na Jumapili ya tarehe 13 Agosti
2017 itakayo ongozwa na Kauli mbiu “Mtakatifu Maria Mama wa Mungu”. Nia ni kutaka
kukumbuka tukio la Mama Maria kuwatokea watoto watatu wachungaji Francisko, Jasintha
na Lucia.
Ikumbukwe kwamba hija inaaangukia ndani ya Wiki ya Kitaifa ya Wahamiaji, kwa njia
hiyo ni kama hija ya wahamiaja na wakimbizi. Tukio wiki ya wahamiaji limefikia mwaka
wa 45 nchini Ureno ambalo limeandaliwa Utume Katoliki kwa ajili ya wahamiaji. Ni
sehemu ya Kamati ya Baraza la Maaskofu ya kichungaji jamii na maendeleo ya binadamu
nchini Ureno. Kauli mbiu ya mwaka huu ni kupokea wakati ujao,kwa vizazi vijavyo
vya wahamiaji ambao ni binadamu wa kesho.
Katika ratiba inayohusiana na hija katika Madhabahu ya Fatima, wataunganika siku ya Jumamosi 12 Agosti 2017 saa kumi na mbili na nusu za jioni , mara baada ya mkutano na vyombo vya habari kuwakilisha tukio. Saa tatu na nusu za usiku katika Kanisa dogo la kutokea Mama Maria,kutakuwa na baraka ya mishumaa na kusali Rosai . Saa nne na nusu usiku itafuatia misa ya kimataifa. Na baada ya misa hiyo itafuatia mkesha wa wa sala na kuabudi Ekaristi Takatifu. Jumapili tarehe 13 Agosti 2017 katika maporokia yote na Jumuiya za kikristo nchini Ureno itakuwa ni siku ya mshikamano.
Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |