2017-08-07 15:59:00

Papa awatia moyo vijana wa Asia kusikiliza sauti ya Mungu


Maadhimisho ya Siku ya Saba ya Vijana Barani Asia kwa Mwaka 2017 yameongozwa na kauli mbiu “Furaha ya vijana wa Bara la Asia: “Kuishi Injili katika wingi wa tamaduni  katika Bara la Asia”. Ni tukio ambalo limeunganisha nchi 21 za Bara la Asia na zaidi ya vijana 2elfu wameshiriki Ibada ya  misa Takatifa ambapo pia aliudhuria hata Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Indonesia Bwana Yusu Kaala. Maadhimisho haya yalifunguliwa rasmi, Jumapili tarehe 30 Julai 2017 ambapo na kufikia kilele chake  tarehe 6 Agosti 2017, wakati Mama Kanisa  anaadhimisha Sherehe ya Kung’ara kwa Bwana.

Katika tukio la kuhitimisha siku  hiyo,  Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake wa  salam na matashi mema kwa vijana wote waliokusanyika katika siku hiyo, ujumbe huo  uliosomwa wakati wa Misa Takatifu, uliotiwa saini na Kardinali Petro Parolini Katibu Mkuu wa Vatican. Ujumbe unawatia moyo vijana kwamba; Baba Mtakatifu anawaombea vijana wote waliokusanyika pamoja huko Yogyakarta nchini Indonesia ili waweze kuwa makini katika kusikiliza  sauti ya wito wa Mungu anaye waita na   kuujibu kwa imani ushupavu katika wito huo. Akiwakumbusha siku ya Vijana duniani itakakayo fanyika mwaka mwaka 2019, Baba Mtakatifu Francisko anasema,  wanajiandaa na Siku ya Vijana duniani; wanawaalikwa kutamtazama Mama  Maria Mama wa Mungu kama mfano wa utume wa kimisonari, vijana hao wapate kuongea naye kama mama na kumwomba daima katika maombezi yake mema. Kwa njia hiyo  wao wawe wafuasi wa Yesu Kristo na zaidi wazidi kufungamana na kijana mwanamke  wa Nazareth . Hiyo itawafanya kuwa wa kweli, kwenda ulimwengu wakiacha ishara zao kwa vijana wengine na familia, kwa njia ya maombezi ya Mama Maria. Amemalizia ujumbe wake na Baraka za amani na furaha kutoka kwa Mungu.


Kwa miaka mitatu ijayo , vijana hawa katika nchi za Bara ka Asia watakuwa wam pata njia zao au  wengine  watakuwa bado ndiyo wanazidi kutafuta. Mwandishi wa Radio Vatican aliongea na Kardinali Luis Antonio Tagle askofu Mkuu wa Manila nchini Ufilippine ambaye pia ni Rais wa Caritas Kimataifa kuelezea Kardinali Tagle amesema, siku hizi za maunganiko ya vijana huko Indonesia zimelenga vijana Barani Asia. Na hii ni kwa mara ya tatu tangu kuanzishwa kwake. Kama   kauli mbiu ya Indonesia imekuwa ni  utume wa vijana katika jamii yenye tamaduni nyingi. Kwa upande wao, kuwa na tamaduni nyingi maana yake pia na  dini nyingi, lakini roho ya makutano na pia roho ya  muungano.Tamaduni nyingi zimunganika na pia dini nyingi kuuganika kwa pamoja.

Roho ya kuunganika ni muhimu kwa ajili ya Kanisa la Asia. Na kwa ajili ya vijana,  ni muhimu kuanza na utamaduni na pia kuwa na  majadiliano ili kuweza kufisifiana utofauti , kwasababu utofauti siyo sababu ya kutengana bali ni utajiri mkubwa ndani ya raia  wa jamii nzima kwa ujumla. Kardinali Tagle pia akitoa ushuhuda juu ya nchi yake ambapo wakatoliki inahesabiwa kuwa siyo wachache, lakini pia kuwa na matatizo yanayohusu mazungumzo ya kidini, na uwepo wa itikadi kali ambazo pia ni kama vile nchi ya Indonesia, amesema, ni mategemeo ya kwamba majadiliano ya kidini yanaweza  kutoke kwa sababu ya historia ya nchi ya Indonesia. 

Historia hiyo ina maana kubwa  kwa bara lote la Asia. Hiyo ni kutokana na kwamba wanzilishi na baba wa nchi ya Indonesa walikuwa wanataka nchi ibaki na makabila mengi na  dini nyingi mahali ambao huru na utambuzi wa kila mmoja ungeweza kuheshimiwa.  Cardinali anasema tumshukuru Mungu hadi sasa roho ya kibinadamu bado ipo katika nchi kubwa , na hii imejionesha na kuleta mafanikio.
Ametoa mfano wa eneo la Mindanao huko Kusini mwa Ufilippine mahali ambapo kuna migogoro ya wanamgambo  wa kutumia silaha, lakini pia anatambua ya kwamba wapo watu wanaotoka Indonesia, ambao ni watu wema. Aidha anao   utambuzi wa hali halisi na ngumu wanayokumbana nayo katika majadiliano ambayo husaidia Serikali ya Ufilippine na watu wa Mindanao.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.