2017-08-05 15:27:00

Caritas nchini Burkina Faso waandaa mpango wa kupambana na njaa


 “ Kom Saaya maana yake njaa imemalizika “ ndiyo moto wa mpango wa mradi wa kupambana na baa  njaa  nchini Burkina Faso iliyotolewa na Caritas mahalia kwa msaada wa Caritas nchini Hispania. Mpango huu unahusisha kwa namna  ya pekee majimbo matatu ya  nchini ambayo ni  Ouahigouya, Dori e Kaya waliokumbwa na baa la ukame. Mpango huo wa Caritas unakaridiriwa kiasi cha milioni 1.2 za kifranki. Mpango wa mradi  wa kazi hiyo unategemewa kufanyika  kwa miaka miwili ambapo unatazama sekta mbalimbali kama vile sekta ya kilimo, ufugaji, mazingira, vyakula, maji safi ya kunywa na huduma za usafi kwa ujumla. Eneo katika jiografia linalihusiana na  eneo lenye umaskini wa kukithiri nchini Burkina Faso. Kwa  miezi miwili ya mwisho wamekumbana na upepo mkali ulio haribu mazao na makazi mengi. Katika Jimbo la Dori,kwa mfano wanawake wanalazimika kutembea km tano kwa ajili ya kuchota maji yaliyo muhimu katika maisha ya nyumbani.

Katika sherehe zilizofanyika wakati wa  kuwasilisha mpango wa mradi huo, Askofu Thomas Kabore’ wa Jimbo la Kaya amesisitizia kukomesha njaa na malengo ya mpango wa mradi kuwa ni changamoto kubwa. Na kufanikiwa kwa mradi huo unahitaji nguvu ya pamoja na kweli kati ya  mtu  na jamii nzima kwa ujumla. Aidha anaongeza kusema kwa dhati kushirikiana watu wote wakiwemo viongozi wa nchi  wa mikoa, wilaya, kata na vituo vyote vya kidini.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.