2017-08-04 14:00:00

Utu na heshima ya binadamu; haki na amani vipewe kipaumbele!


Hakuna kushindwa katika kutafuta namna ya kuwezesha majadiliano katika nchi ya Venezuela. Ameyasema maneno hayo Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akihojiwa na gazeti la Baraza la Maaskofu Katoliki la “Avvenire”. Kardinali Parolin anasema, Diplomasia ya Vatican ni diplomasia ya amani. Haijihusishi na maslahi ya kisiasa, kiuchumi hata kiitikadi. Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha kuwa wanapojikuta mbele ya kipeo cha namna fulani ni lazima kufikiria namna gani  Vatican itoe huduma. Kwa njia hiyo ni diplomasia inayotenda na siyo inayosimama na ndiyo maana wanatafuta namna ya kupeleka mshikamano ila inapowezekana. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Vatican, anasema , iwapo wakati mwingine inashindikana, la muhimu ni kuendelea kutoa na kufanya matendo ya dhati, kwa njia hiyo huweza kusema  hiyo ni kushindwa.Kwa upande wa nchi ya Venezuela, mtazamo wake ni kwamba inawezakana kuwapo maoni tofauti, lakini muhimu ni kutafuta namna ya kupata majibu yanayowezakana kulingana na hali halisi hasa kwa kufikiria watu na kwa ajili ya manufaa ya wote ambayo ndiyo inapaswa kupewa kipaumbele.


Pamoja na kuongelea juu ya nchi ya Venezuela, Katibu Mkuu Parolin pia ameitaja hali halisi ya nchi ya Colombia ambapo amesema ni matumaini yake kuwa udhaifu na matatizo yaliyopo yanaweza kutatuliwa  au kuhimarishwa hata  kutiwa moyo kwa sababu ya ziara ya Baba Mtakatifu Francisko anayotarajia. Anaongeza kusema, Baba Mtakatifu Francisko anataka kutembelea nchi ya Colombia kwa lengo la  kuhamasisha maridhiano na amani. Katika nchi za Kusini mwa Marekani zinatakiwa maridhiano na amani ili ndani ya nchi hizo ziweze kufikia msingi wa kina na kuanza safari ya ukomavu wa amani kamili kutokana na uwepo wa mgawanyiko hata wa kisiasa.

Akizungumzia kuhusu vurugu za nchi za Mashariki katika Gazeti hilo la Avvenira, Kardinali Parolini anasema, hali ya vurugu za nchi hizo nazo ni zinatia wasiwasi, ni lazima kujibidisha ili kufikia amani ya kudumu. Anathibitisha kusema kuwa, nazo nchi za Mashariki  ziko kwenye mboni ya macho ya Vatican. Leo hii hali inazidi kuongeza wasiwasi mkubwa, pamoja na kwamba Vatican inatambua Yerusalem ni sehumu mojawapo Takatifu wa wayahudi , wakristo na waislam. Yerusalem ni mji na makazi ya watu wote waamini, ni mji ulio wazi  kwa maana ya kutambua uhuru wa dini na haki zake ambazo zinaheshimiwa. Kwa njia hiyo Kardinali Parolin anasema, iwapo inaongezeka wasiwasi ni lazima kutafuta namna ya kuzuia migogoro hiyo.Lakini kuna tatizo  lenye mzizi wa kina ambalo ni moja yaani inahitajika utashi kisiasa.

Katika ngazi ya kimataifa anasema wanaweza kuzungumzia juu ya kutafuta mbinu za kutatua matatizo na  uwezekano   hu kweli upo kwa maana ya kwamba, kuna uwezekano wa kujibu katika kutoa maoni kamili ambayo yanaweza kweli kuwa yenye mwafaka, anasisitiza akisema  kwa bahati mbaya  hali hii inaonesha kuwa na ukosefu wa utashi, yaani kila mmoja kuweka kile alicho nacho au kuahidi. Kwa upande wa maoni ya  Kardinali Parolini, kinachobaki  hakika ni  kupendekeza sheria ya kulinda sehemu zote za kihistoria na dini Yerusalemu pia uwepo wa huru wa mtu  kwenda maeneo matakatifu. Maandamano ya vurugu  ambayo huonekana yataka kusema kwamba tatizo linapaswa kutatuliwa katika ngazi ya kimataifa.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.