2017-08-03 15:01:00

Vijana wa Jimbo Vorarlberg Austria kufanya uzoefu na vijana wa Ethiopia


Caritas nchini Austria inashirikiana na mipango ya kijamii nchini Ethiopia kwa miaka 15 hivi katika majimbo Katoliki ya Addis Abeba na Meki, ambapo kila majimbo ya Austria yanawawezesha vijana  kwenda katika nchi ya Ethiopia kufanya uzoefu wa mshikamano. Na hii imejitokeza hata katika Jimbo la Vorarlberg nchini Austria ambapo vijana 13 wa kike na kiume wamerudi kutoka nchini Ethiopia hivi karibuni  baada ya kufanya uzoefu wa wiki tatu. Moja ya mipango mitatu, walipanda miti ya maembe katika familia 60 kwenye vijiji. Na   pia vijana hawa wa Austria walijengea  miembe  hiyo  miti ya miiba ili kuzuia mbuzi wasile miti ya miembe  iliyopandwa. Kila familia iliweza kupewa miti minne ya maembe ambayo watawajibika kuitunza katika kumwagilia maji.

Akielezea kwa nini waliamua kupanda miti ya miembe Lea Fellacher mmoja waapo katika kundi la kujitolea anasema, faida  ya miti ya miembe ina nguvu na hutoa matunda mengi ambapo inaweza kuwanufaisha wanafamilia kupata matunda ya kutosha. Mpango mwingine wa fedha za Caritas wa  Jimbo la Vorarlberg umetumika  katika ujenzi wa Vyoo vinne kwa ajili ya utunzaji wa  afya bora  katika mashule. Vijana hawa 13 wa kujitolea  walikuwa wamejiandaa kikamilifu na michoro yao ili kuweza kuwafundisha  watoto wa shule ubora na umuhimu wa kutumia vyoo na usafi wa mazingira kwa ujumla hasa kwa kuzingatia kuanzia usafishaji wa mikono.

Mpango  mwingine wa nne ulikuwa kuwahusisha vijana zaidi ya 45 katika mafunzo ya ujana kuanzia miaka 11 hai 16 ambapo walijadiliana kwa kina juu ya matatizo ya ujana na matatizo mengine mengi yanayo husu afya. Vijana wa Austria wakisaidiwa na viongozi mahalia wamefanya kila njia ya kuweza kuwaunganisha vijana hawa na wageni, kujifungua zaidi na kuwa wazi katika kushirikishana uzoefu wao na uzoefu wa vijana wa Ethiopia na njia hii imewapa vijana fursa ya kujuana na kushirikishana. Naye Askofu wa Jimbo la Meki Abraham Desta  wakati wa kuwaaga  alizungumzuia juu ya faida za mshikamano wa vijana kutoka Austria na kwamba wameweza kuvunja ukimya na kuonesha juhudi zao kama vijana, aidha tendo la  kushirikishana matatizo yao na watu wa nje ni fursa pia ya kueleimika zaida katika kubadilishana uzoefu na kueneza mshikamano .

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.