2017-08-03 15:32:00

Ni zaidi ya wakristo milioni 14.5 katika nchi zote za Mashariki


Ni watu zaidi ya milioni 14.525.880 wakristo katika nchi za mashariki wanaoishi kati ya  Cyprus, Misiri , Iraq , Israeli, Jordan, Lebanon, Cisyordania, Gaza, Siria, Uturuki  na katika mji wa Yerusalem. Ukiunganisha nchi pamoja ni  karibu milioni 258 za wakazi. Hii ni takwimu iliyotolewa katikati ya mwaka 2017 ikionesha pungufu ya waamini wakristo 213,780  ukilinganisha na ile ya mwaka 2010 ambapo wakristo walikuwa 14.739.660.

Ni ripoti ya Shirika la Ustawi Katoliki wa chi za Mashariki (Cnewa).Shirika hili lilianzishwa na Baba Mtakatifu Pio wa XI mwaka 1926 kwa ajili ya kusaidia binadamu na utume kichungaji  kwa watu masikini wa nchi za Mashariki, Afrika ya kaskazini Mashariki, India na Ulaya ya mashariki. Ripoti hiyo iliyotolewa inaonesha maendeleo ya wakristo wa nchi za mashariki katika mwanga  wa shughuli zote za kanda katika miaka ya hivi karibuni na hasa  kwa kuonesha vita nchini Siria na Iraq, kuundwa  kwa Serikali ya kiislam ambayo imeharibu tamaduni katika nchi ambazo wakristo wake wamelazimika  kukumbilia uhamishoni kwenye nchi nyingine au kuishi wamerudikana sehemu moja  zilizo karibu.

Nchi ya Iraq ni kati ya nchi iliyonukuliwa upungufu wa wakristo kutokana na vita na ghasia za dini iliyokumba nchi nzima, hata kiuchumi na kisiasa. Katika miaka ya 90 waamini wakristo walikuwa zaidi ya milion moja. Kwa mwaka 2016 wamekuwa wakihesabiwa kwa shida watu 300 elfu. Mwaka 2016 baada ya kushambuliwa na Serikali ya Kiislam katika maeneo ya Ninawi, wakristo walio rundikana  Kurdistan na katika nchi jirani  kama Jordan, Uturuki na Libanon, kwa mujibu wa Shirika hili ni watu 140 elfu na pia  50 elfu ni  wale walio acha nchi zao . Hali kadhalika ripoti inasema nchini Siria kutokana na vita vilivyoanza 2011 wakristo wamepungua kutoka milioni 2,2 mwaka 2010 kufikia wakristo milioni 1.1 mwaka 2017. Maelfu na maelfu ya wakristo wameacha nchi yao. Hata hivyo mizizi ya Kanisa nchini Siria imesimikwa na maisha ya jumuiya ya parokia mahalia inayozidi kuwendela kuwapo, ni matumaini ya wengi kwamba mambo ya naweza kubadilia ili wakristo wengi walioko uhamishoni kurudi makwao.

Na kwa upande wa Misri ni nchi ambayo wanaishi jumuiya kubwa ya wakristo wa nchi za mashariki milioni 9,4 ya waamini ambao ni asilimia 10 ya jumla yatu Wakoptik. Taarifa ya (Cnewa) inasema kuyumba kwa siasa na uchumi ni mambo mawili yaliyounganishwa na kusababaishwa na hali ya vurugu na uzushi wa dini mbalimbali zitokanazo na dini ya kiislam dhidi ya wakristo ambao kwa sasa wameona makanisa 76 yanachomwa hovyo wa miaka ya hivi karibuni. Tangu mwaka 1910 hadi leo wakristo wamepungua nusu kutoka asimia 20 hadi asilimia 10 ya watu. Walio wengi ni wakoptik walio acha nchi yao na kuhamia katika nchi za Canada na Marekani.

Katika nchi ya Israeli , ripoti inaeleza, leo hii wanahesabika wakristo 170 elfu , na sehemu kubwa ni waharabu wa Israeli.Hao wanawakilisha asilimia 2.4 ya jumla ya wakazi. Mwaka 1948 mwaka uliozaliwa nchi ya Israeli, wakristo walikuwa wanafikia asilimia 20. Lakini baada ya kuanza vurugu za Waarabu wa Israeli, Wapalestine wenye imani ya kikristo waliacha nchi yao. Leo hii kuna waamini wa kimelkit, waorthodox, walatin , warmenia, na wamaroniti walio hama kutoka umoja wa kisovietic. Hawa walifikia nchini Israeli  kwa sheria ya kurudi 1950.Katika ripoti inasemeka ni zaidi ya watu 300 elfu na kati yao ni waorthodox; Lakini pia kuna waamini 60 elfu kati yao ni waeritrea, waethiopia, wafillippini, wahindi , wa kutoka Marekani ya kati ,Waroma na Wamoldavi sehemu kubwa ni wakristo. Uwepo wa wakristo huko Yerusalem ni waamini 15,800 kati ya 870 elfu ya wakazi  wengi kutoka Palestine  wenye imani ya kikristo.

Jordan kwa sasa inakadiriwa kuwa na wakristo 350 elfu ambao ni zaidi ya asilimia 2.2 ya watu sehemu kubwa ni waislam wa kisuuni. Kutokana na vita nchini  Siria,  Iraq na uwepo wa kikundi cha kigaidi cha Isis, Ufalme wa nchi hiyo kwa miaka mitatu (2014-2017),wameingia zaidi ya watu 30 elfu wakristo kutoka Iraq na familia elfu moja wamehama na kwenda kuishi nchi ya Astralia na Canada pia. Nchi ya  Libanon kwa mwaka 1932 karibu nusu ya watu walikuwa wakristo. Leo hii wakristo ni kama asilimia 40 ambayo ilikuwa milioni 2 kwa mwaka 2010.Kutokana na kuongezeka kwa wakimbizi wengi kutoka Siria na ukosefu wa ajira,imesababisha watu wengi wa Lebanon kuhamia nchi za nje.


Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.