2017-07-21 16:34:00

Askofu Philipp Pollitzer ang'atuka madarakani


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Philipp Pollitzer wa Jimbo Katoliki la Keetmanshoop nchini Namibia, la kung’atuka kutoka madarakani baada ya kulitumikia Kanisa kama Askofu kwa muda wa miaka 10 na Padre kwa muda wa miaka 59! Itakumbukwa kwamba, Askofu Philipp Pollitzer alizaliwa kunako tarehe 18 Januari 1940, huko nchini Austria.

Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa na kipadre, kunako mwaka 1960 akaweka nadhiri zake za daima na hatimaye, kupewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 17 Desemba 1965. Akaendelea kuchapa kazi sehemu mbali mbali hadi kunako tarehe 31 Mei 2007, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Keetmanshoop nchini Namibia na kuwekwa wakfu hapo tarehe 14 Julai 2007. Na Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 21 Julai 2017 akaridhia kung’atuka kwake kutoka madarakani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.