2017-06-16 17:22:00

Padre Bruno Marie Duffè ateuliwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Bruno Marie Duffè kutoka Jimbo kuu la Lyon, Ufaransa, kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu. Ni muasisi mwenza na mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Msingi za Bibadamu, Chuo Kikuu Cha Kikatoliki cha Lyon na Jaalimu wa Maadili Jamii na Afya katika Taasisi ya Lèon Bèrard ya Kupambana na Saratani, huko Lyon, Ufaransa.

Mheshimiwa Padre Bruno Marie Duffè alizaliwa kunako tarehe 21 Agosti 1951 huko Lyon, nchini Ufaransa. Kunako mwaka 1981 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kunako mwaka 1996 akatunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Falsafa, Haki Msingi za Binadamu na Maadili Jamii. Kunako mwaka 1982 hadi Mwaka 2005 amekuwa akifundisha Taalimungu maadili na Mafundisho Jamii ya Kanisa kwenye Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Lyon na katika Taasisi ya Lèon Bèrard ya Kupambana na Saratani. Amechangia kwa kiasi kikubwa kuanzisha kwa kitengo maalum cha haki msingi za watoto kwenye Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO. Kwa sasa ni mshauri wa masuala ya kiroho kwa wafanyabiashara wa Kikatoliki nchini Ufaransa. Ni mwandishi mahiri wa vitabu na makala mbali mbali hasa kuhusiana na haki msingi za binadamu, wakimbizi na wahamiaji. Amewahi kuwa mshauri wa masuala mbali mbali katika Umoja wa Umoja.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.