2017-06-03 14:07:00

Balozi George Johannes awasilisha hati za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi, tarehe 3 Juni 2017 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa GeorgeĀ  Johannes, Balozi wa Afrika ya Kusini mjini Vatican. Anakuwa ni Balozi mkazi wa kwanza kutoka Afrika ya Kusini, ameoa! Kitaaluma , ana shahada ya uzamivu katika falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza pamoja na shahada ya uzamili katika masuala ya siasa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Birbeck, Uingereza.

Katika masuala ya kisiasa, kunako mwaka 1995 aliteuliwa kuwa ni Mkurugenzi wa mahusiano ya kimataifa katika Idara ya Kazi, Chama cha A.N.C. Kunako mwaka 1997 akahamishiwa Idara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, DIRCO. Mwaka 1997 hadi mwaka 2003 akateuliwa kuwa ni Kaimu Kamishina wa Afrika ya Kusini nchini Uingereza na Canada. Mwaka 2004- 2009 aliteuliwa kuwa ni Kaimu Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Ujerumani. Na kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 20014 alikuwa ni Balozi wa Afrika ya Kusini mjini Vatican na Liechstein.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.