Baba Mtakatifu francisko Jumanne 30 Mei 2017 amewapokea na kuzungumza na Maaskofu
wa Albania ambao wako kwenye hija ya kitume,katika mkutano wao wameonesha matumaini
kwako ya Kanisa dogo la nchi hiyo. Katika moyoni mwa Papa Kanisa la Albania linayo
nafasi maalumu kwasababu ni Kanisa lililotesaka sana: kwa miaka 50 chini ya udikteta
wa kikomunisti ambao ulitafuta kwa namna moja au nyingine kufuta Kanisa hilo lakini
ikashindikana,hata hivyo ziara ya Baba Mtakatifu haitasahulika ya kutembelea nchi
hiyo mwezi Septemba 2014.
Katika ziara yake hiyo aliwaalika waamini wa Kanisa Katoliki waruke kama tai ambayo
ni ishara iliyoko katika bendera ya taifa , lakini pia wasisahau kiota cha ndege
huyo ikiwa na maana ya kutosahau mateso ya mashahidi wa nchi hiyo. Kwa njia hiyo mwezi
Novemba mwaka jana mashahidi 38 walitangazwa kuwa wenye heri. Hata hivyo katika mazungumzo
nao Baba Mtakatifu Francisko amesisitizia kuiga mfano wa mashahidi hao wa Injili
waliolipa nafsi yao kwa ajili kutetea imani yao katika Kristo.
Ili kuelezea Mkutano wa maaskofu wa Albania na Baba Mtakatifu, Askofu Mkuu wa Scutati Angelo Massafra na Rais wa Baraza la Maaskofu amesema, imekuwa uzoefu mzuri wa kukaa na Baba Mtakatifu wakijadiliana kwa pamoja katika kupewa nafasi ya kuongea nao bila haraka kwa utulivu,na kwamba kweli wamejisikia kupokelewa vizuri utafikiri walikuwa nyumbani kwao. Askofu amaeleza jinis walivyozungumza kuhusu kukua kwa Kanisa lao japokuwa ni maskini na shahidi ambapo Baba Mtakatifu amewashauri waendelee mbele kwasababu Kristo amefufuka na wao ndiyo wako mstari wa mbele kutangaza hilo. Aidha amewaalika kuhamasha miito akisisitiza kuwa shughuli za kichungaji dama zijikite hawali ya yote kupitia ushuhuda. Zaidi amewashauri wawe na umoja katika yao na kuwa na utulivu pia furaha kwasababu ya utambuzi kwamba mwenye furaha ugeuka kuwa mfano kwa wengine.
Alikadhalika wamegusia juu ya majadiliano ya kidini , ambapo wamemweleza juu ya
wiki iliyopita kuweka makubaliano kati ya nguvu za serikali na wapinzani wake: kama
wajibu wa Kanisa kwa umma wameweka nao mkataba wa pamoja kati yadini tofauti yaani
wakatoliki, waorthodox ,Waluteri , waislam na, bektashi mkataba huo wa pamoja ni wa
kupinga machafuko na vurugu , ili kukaribisha ushirikiano, mshikamano na majadiliano.
Ni Mkataba wa umoja wa Baraza la kidini ambapo Baba Mtakatifu Francisko amefurahishwa
juu ya hilo. Amwewashukuru maaskofu kwa mchango wao kwani umewawezesha nguvu za kisiasa
kuwa na makubaliano ambayo wameamua kupeleka mbele tarehe za uchaguzi mkuu ili kuwezesha
wote waweze kushiriki. Kwa njia hiyo askofu anasema hilo ni tunda la nguvu za Kanisa
katika shughuli za majadiliano ya kidini na kiekumene.
Matarajio ya Kanisa la Albania baada ya Mkutano na Baba Mtakatifu Askofu Mkuu Angelo anasema ni kwenda na kutoa ujumbe msingi ambao baba Mtakatifu amewahimiza yaani wa kuwa na umoja kati yao,kujibidisha katika utume wa wafamilia na maskini. Anaongeza kwamba katika Kanisa la Albania walikuwa tayari wanapeleka mbele shughuli za wafungwa na familia zenye waleamavu.Kwa njia hiyo maneno ya Baba Mtakatifu yanatoa msukumo zaidi na kuwaalika jamii nzima ya Albania kuwa na matumani, pia kusali na kuabudu Yesu wa Ekaristi , maana kwa njia ya Kristo tunaweza kwenda katika upeo endelevu anasema Askofu Mkuu Massafra na pia anabainisha kuwa,Papa amewatia moyo na kuwabariki.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |