2017-05-30 15:04:00

Papa:Wachungaji wajifunze kuaga zizi lao na kwenda kwingineko!


Mchungaji wa kweli  anajua vema namna ya kuaga vizuri Kanisa lake, kwasababu  anatambua kuwa yeye siyo kiini cha historia bali ni mtu huru anayetoa huduma bila kuvutia kwake na  bila  kujinufaisha yeye binafsi zizi hilo. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake Jumanne tarehe 30 Mei 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican. Kiini cha mahubiri yake kimetokana na somo la kwanza kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume , ambapo Baba Mtakatifu anatafakari juu ya Askofu kuaga zizi lake kwa maana ya  Mtakatifu Paulo akiwaaga Jumuiya ya  Kanisa la Waefeso, Kanisa ambalo ndiye mwenyewe aliye lianzisha na sasa anaondoka. 

Wachungaji wote lazima waage, maana inafikia kipindi ambacho hata Bwana alisema: anakwenda sehemu nyingine, kwenda huko na kule. Na hiyo ndiyo hatua moja ambayo kila mchungaji lazima kujiandaa kuondoka vizuri na siyo kuaga nusu. Baba Mtakatifu anabainisha kwamba, mchangaji asiyejifunza kuaga na kuondoka ni kwasababu anayo mahusiano yasiyo mazuri na zizi lake, hayo ni mahusiano yasiyo safishika katika msalaba wa Yesu.
Anafafanua kuwa, Mtakatifu Paulo aliwaita  makuhani wote huko Efeso kwa maana nyingine ni kusema  kama vile mtaguso wa makuhani na kuwaaga. Ili kuwelezea vizuri jambo hilo, amebainisha aina tatu za kitume.

Hawali yayote anasema kama mchungaji usirudi nyuma kamwe: na  hiyo siyo kitendo cha ubatiri kwasababu Paulo anasema hiyo ni dhambi kubwa kwani anatambua na ndiyo maana anasema hivyo kutokana na historia inavoelezea juu yake.
Baba Mtakatifu anasema kwa dhti hiyo ndiyo mojawapo ya  amani atakayokuwa nayo wachungaji anapowaaga watu wake ka namana hiyo. Aidha Paulo alikuwa mchungaji asiye jiingiza katika tuhuma wakati wa kuongoza Kanisa kwasababu alikuwa akitambua wazi kwamba hakuongoza kwa njia ya kujivutia kwake nhata hakurudi nyuma, kwa njia hiyo inahitaji ujasiri Baba Mtakatifu anasisitiza.

Sehemu ya pili ya utume wa uchugaji , Paulo anasema alikwenda Yerusalem kwa kulazimishwa na Roho bila kutambua nini kitatukia. Yeye aliamini na kufuata Roho hiyo , kwa namna hiyo mchungaji anatambua vema kuwa hiyo ni safari: Wakati akiwa anaogoza Kanisa Paulo alikuwa na tabia ya kutojiweka matatani; lakini kwa sasa Roho inamtaka ajikite katika safari bila kujua litakalomtukia. Yeye anaendelea kwasababu hana linalomzuia kama mali yake,anao utambuzi kuwa  siyo yeye aliyeunda zizi hilo na kwamba analo deni. Yeye anatoa huduma tu. Kwa namna hiyo Mungu anataka aende, na hajuhi nini litatukia kwake anachotambua kutokana na roho ni kwamba kila mji uliokuwa unamsubiri ni minyororo na mateso.
Kile alichokuwa anatambua ni kwamba haendi pensheni Baba Mtakatifu anaeleza, Anakwenda hasikojua kutumikia Kanisa lingine.Yeye alikuwa daima akimfulilia moyo sauti ya Mungu. Hiyo inafundisha namna ya kufungua miyo na kuaacha jisni ilivyo ili kuona Bwana anataka nini. Na ndicho hicho bila tuhuma zozote Paulo  anakuwa mchungaji  katika mwendo.

Baba Mtakatifu ameelezea pia  kwanini huwezi kubinafsisha zizi ambayo ilikuwa ni sehemu ya tatu ya maelezo  ya hudma ya kichugaji kwamba, yeye mwenyewe anaamini kila aina ya tunu ya maisha iwe kubwa au ndogo ya utume ni kiini cha historia.  Anatoa mfano wa msemo wa watu wengi wasemavyo kuwa jinsi  unayoishi ndivyo  unavyokufa , jinsi unavyoishi ndivyo unavyoaga. Kwa maana  hiyo Paulo anaaga akiwa na uhuru wakea bila kujiingiza matatani na anaendelea na safari, hivyo ndiyo inavyotakiwa kwa kila mchungaji. Anamalizia akisema Baba Mtakatifu kuwa, katika mfano huo mzuri , tusali kwa ajili ya wachungaji wote ikiwa ni maparoko maaskofu , papa ili maisha yao yawe ni maisha huru yasiyo na majivuno , yawe maisha ya mwendo na maisha ambayo siyo kijiaminisha kwamba wao ni kiini cha historia bali  wajifunze kuaga vizuri.Tusali kwa ajili ya wachungaji!

Sr Anela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.