2017-05-30 16:54:00

2017 Shirika la Mt. Vincent wanaadhimisha miaka 400 ya karama yao


Kwa ajili ya tukio madhimisho ya miaka 400 ya kuanzishwa kwa Shirika la Mtakatifu Vincent  , wana w ana wa upendo wanao ishi na kutoa huduma katika nyumba na  Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini watatoa zawadi ya nishani ya miujiza kwa wote watakao udhuria misa ya kufunga mwezi wa Maria Mjini Vatican. Kama utamaduni wa kila tarehe 31 Mei kuanzia saa mbili usiku,watasali rosari wakiwa katika maandamano wakiwa wameshika mishumaa hadi kufikia katika groto la Maria wa Lourdes.Mwandishi wa Habari wa Radio vaticana amekutana ka kuhojiana na Sista Stefania Monti mama Mkuu wa Shirika la watoto wa Upendo wanao hudumia nyumba ya Mtakatifu Marta Mjini vatican, kuelezea juu ya maandalizi ya kufunga mwezi wa Maria na pia kuhusa tukio la miaka 400 ya karama yao ya Shirika.

Sista Stefania anaelezea kuwa, kuwakabidhi nishani ya Maria wa miujiza washiriki wote  katika hija ya maombi wakati wa kumalizia mwezi wa Mama Mamria ni kutaka kuthamanisha zawadi hii ya Bikira Maria Mtakatifu aliyofanya kwa Mtakatifu Caterina Labouré , hata kwa ajili ya shirika lote. Ni ishara kubwa ya wema wa Mungu kwa binadamu wote. Hata hivyo ishara hiyo inajihusisha zaidi kwani ni moja ya  maadhimisho muhimu kwasababu Familia ya Mtakatifu Vincent inaadhimisha miaka 400 ya karama hii. Ni tukio linalowakilisha wanafamilia wote , wamisonari wa upendo na vyama vyote vya upendo ambao leo hii bado wanajikita katika utume. Aidha anaongeza kusema,hiyo ni  karama inayoonesha njia ya huduma, na  ni kama papa anavyopendelea kusema daima, kwamba ni familia ya inayotoka nje kwenda njiani. 

Akielezea  hata mipango mingine iliyoandaliwa kwa ajili ya tukio  la miaka 400 ya karama kwamba, wao kama watoto wa upendo wanao toa huduma katika nyumba ya Mtakatifu Marta , wamendaa  mipango ya aina mbili ya kindugu kwa wote wanaoishi katika nyumba hiyo (Sanctae Marthae).Na wakati wa mkutano wao waliongelea kuhusu Mtakatifu Vincent, Mtkatifu wa upendo na zaidi wamefanya uzoefu wa kutazama kwa kina ni  jinsi gani ya ilivyo vema  kuishi kwa pamoja, wakishirikishana kila mmoja uzoefu wa maisha ya familia. Halikadhalika akijibu swali juu ya jubileo ya karama ya Mtakatifu Vincent inawasaidia je na hasa wao katika kutoa huduma kwa namna ya pekee katika nyumba ambayo Baba Mtakatifu Francisko anaishi; Sista anasema, kiukwelini ni huduma ya pekee ambayo hata wao wenyewe wanarudia kusema kila siku! Ni huduma ambayo wanaishi katika Kitovu cha Kanisa wakiwa na  Khalifa wa Kristo ambaye ni Papa Francisko. Kwa njia hiyo mwaka 2017 wanaishi kama kipindi cha neema ya  pekee na msingi mkubwa kwa ajili ya Shirika lao. Ni miaka 400 Karama hii inaendelea kutembea anjiani katika ulimwengu na mioyo yao  ikiwa inawaka mapendo kwa watu  wengi  ambao wanakutana na kutoa huduma.

Aidha amemalizia kujibu swali juu ya uwepo karibu nao wa Baba Mtakatifu katika matukio mengi na ishara za upendo hasa wakati wa misa za kila siku katika Kanisa la Mtakatifu Marta  pia katika kumbu kumbu ya Watakatifu Luisa na Vincent waanzilishi wa Shirika lao,  kwamba daima Baba Mtaktifu Francisko amekuwa akikumbuka katika ibada zake za misa, hasa zaidi inapokuwa ni kumbukumbu za watakatiu hao, katika utangulizi wake anataja kuwa misa hii tunaadhimisha kwa ajili ya wana wa upendo wanaohudumia katika nyumba ya Mtakatifu Marta.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.