2017-05-29 12:14:00

Papa: Je nina uwezo wa kutafakari,kusema kabla ya kutoa uamuzi?


Je mimi ninao uwezo wa kusikiliza ? je mimi ninao uwezo wa kutafakari, kusema neno au kufanya jambo lolote kabla ya kutoa uamuzi?. Ni maneno yake Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri  asubuhi ya Jumatatu 29 Mei 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican.  Baba Mtakatifu Francisko akitafakari neno  la Mungu kutoka Injili ya siku iliyosomwa  amesema, Je moyo wangu umetulia bila kuwa na wasiwasi, yaani kuwa na moyo ulio makini?. Anabainisha  kuwa baadhi ya mioyo kama kungekuwapo na kipima roho, matokeo yake yasingekuwa mazuri maana kuna roho zenye wasiwasi.

Aidha anafafanua zaidi kuwa, hata katika Injili tabia hizi zinaonekana ,kwa kufikiria waandishi wa sheria, kwamba walikuwa wanaamini Mungu na walikuwa wanatambua amri za Mungu. Lakini mioyo yao ilikuwa imefungwa na kusimama, hawakuwa na utayari na wala kutingishika. Kwa nji hiyo Baba Mtakatifu Francisko anatoa ushauri kuw ni vema kuachia kutingishwa na  Roho Mtakatifu. Ametoa mifano kuwa, badala ya wengine kusema Baba mimi nimejisikia hivi je labda huo ni wepesi wa mvuto wa kimoyomoyo?, anaseme haiwezekani kuwa na mvuto tu wa kimoyomoyo na hasa  iwapo unatembea katika njia ya haki; haiwezekani kabisa kuwa ni mvuto wa kimoyomoyo tu. 

Haiwezekani kwasababu kama unajisikia mtu wa kwenda kumtembelea mgonjwa, kubadili maisha au jambo fulani,hizo ni hisia za ukweli wa kufanya mang’amuzi.  Kufanya mang’amuzi kwa kile unacho hisi ndani ya moyo wako, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa inatokana na nguvu ya Roho Mtakatifu ambaye ni mwalimu wa mang’amuzi. Mtu yeyote asiye jisikia mzunguko au mtikiso  wa namna hiyo katika moyo wake, yaani asiye weza kutambua  kile kinachotukia, ni mtu mwenye imani baridi, ni mwenye imani ya kiitikadi. Baba Mtakatifu anaongeza , imani yake ni ya kiitikadi, hakuna jingine. 

Amemalizia kwa kuwataka wajiulize maswali iwapo wanaoomba kuongozwa katika  njia ya haki na kufanya uchaguzi wa maisha ya kila siku, aidha kama wanaomba kupewa neema ya kutambua  yaliyo mema na mabaya,kwa maana kwamba, daima mema hujitenga haraka na ubaya. Lakini wakati huo huo upo ubaya ambao umejificha zaidi ya wema .

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.