2017-05-26 15:36:00

Maaskofu Uswiss: Tuwakaribishe wahamiaji maana ni ndugu zetu!


Wakristo na wayahudi wataungana pamoja katika maombi kwa ajili ya utetezi na ulinzi wa wahamiaji. Madhimisho haya yatafanyika Jumamosi na Jumapili ya tarehe 17 na 18 Juni 2017 nchini Uswiss. Haya ni maandalizi yanayotayarishwa na Baraza la maaskofu wa Uswiss(Ces), Makanisa ya kikristo pamoja na Shirikisho la Jumuiya  Wayahudi. Lengo lake ni kujenga madaraja na mshikamamo kwa ajili ya wakimbizi na watu wote wanaoteseka. 

Yote yanaanzia jumapili muhimu kwa kutazama wahamiaji ambao ni viumbe wa Mungu na ndugu zetu badala ya kuwatazama kama matatizo ya jamii. Ni maneno yaliyotakwa na mmojawapo wa viongozi wanaofanya maandalizi ya siku hizo mbili Rais wa Baraza la Maaskofu wa Uswiss (Ces) Charles Morerod. Anasema kwamba anatambua wazi jinsi  ilivyo ngumu kushinda matatizo ya aina ya  uhamiaji wa kulazimishwa, lakini licha ya hayo  bado kuna sababu ya kuwa na matumaini ya mabadiliko.

Kwa njia hiyo Rais wa Baraza la Maaskofu la Uswiss anatoa  wito  kwamba watu wote  wasiwe na woga dhidi ya wakimbizi bali waonesha matendo ya dhati kama vile kwenda kukutana nao, hata kama hawawajuhi na wala kujulikana, ili kuwapa neno. Anaongeza, mahali ambapo hatua ndogo ukamilika ndipo kuna makaribisho ya kibinadamu ambayo hutoa ule mtazamo wa karibu badala ya umbali na hapo ndipo Mungu yupo.

Sr Angela Rwezaula
 Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.