2017-05-26 14:47:00

25 Mei ni Siku ya Afrika Duniani kukumbuka Umoja wa Afrika


Tarehe 25 Mei  ilikuwa siku ya Afrika duniani ambapo maadhimisho ya Siku ya Afrika kwa mwaka 2017 yamejikita kwa namna ya pekee katika  masuala ya uhamiaji kama sehemu kuu  ya mchakato wa kutaka  kukuza na kudumisha misingi ya ufahamu mzuri wa kuishi katika maeneo mahali na kulima badala ya kuhama na kujikuta katika matatizo makubwa zaidi.Siku hiyo imekuwa na  kauli mbiu "kwanini msibaki". Katika Ripoti iliyotolewa na Shirika la Green Cross , wamefanya utafiti wa matukio ya wahamiaji kutoka nchi ya Senegal. Taarifa hiyo inasema kwamba kutoka Senegal wahamiaji hasa wanaume kuanzia miaka 30 na 50 ni wengi sana ambao hawa elimu au kama wanayo ni ya ngaziya chini.

Kwa maana nyingine hata kama hawana kazi ya maofisini ya kuleta kipato kila mwezi au chochoto cha kula nyumbani , wote wanafanya kazi kwasababu kabla ya kuondoka nchini kwao, walikuwa wakulima japokuwa kilimo kisicho waletea manufaa yoyote bali kuendelea kuishi katika umasikini. Na ndiyo maana wahamiaji hawa wanachagua kuelekea nchi za Ulaya hasazaidi  Ufaransa na nchi za Afrika ya Kati kama vile Gabon,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Italia. Sababu hizo  za kuhama nchi yao ambazo ni kiuchumi, ambapo uondoka wakiwa na matarajio ya kupata mafunzo na baadae kuweza kurudi makwao. Kauli mbiu iliyotolea na ripoti 2017 kuwa kwa nini msibaki ni utafiti kuhusu matukio kuhama watu katika vijini vitano vya Mkoa wa Matam, kaskazini mwa Senegal , iliyo wakilishwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Green Cross nchini  Italia katika tukio la Siku ya Afrika duniani inayoadhimisha kila ifikapo tarehe 25 Mei ya kila mwaka.

Utafiti huo umefanyika  kwa juhudi za mpango madhubuti unao fadhiliwa na Shirika lisilo kuwa la kiserikali  la Italia kwa ushirikano wa Shirika la Maendeleo(AICS) wakiwa  na lengo la kupambana na uhamiaji usio halali na kusaidia kukuza maendeleo ya kilimo endelevu. Takwimu zilizokusanywa na Shirika hilo linabaniisha kwamba wamefanya mahojiano na familia moja kwa moja 564 katika vijiji vinavyofadhiliwa ambavyo vinahusishwa katika kilimo, na kwamba mtu mmoja kati ya famila 10 ameondoka ndani ya familia yake kwenda nchi za nje.
Kwa maana, sababu kubwa ya kuondoka ni kutokana na umasikini , kwani familia nyingi hasa wanaume wanashindwa kuvumilia kuona nadani ya nyumba hakuna chochote na umaskini wa kila kitu; kwa njia hiyo wanaume wanakwenda kutafuta maisha bora ya familia zao. Katika kuhakikisha hili, tarifa inasema asilimia 90% ya watu waliohojiwa wanasaidiwa kifedha kutoka kwa ndugu zao walio hamia nchi za nje kwa ajili ya matumizi ya dawa, chakula, shule, fedha za kulipa kodi za nyumba au umeme.

Aidha  mahojiano yaliyofanyika na vijana wengi wahamiaji inaonesha jinsi gani vijana na wanaume wako radhi kupambana na safari ngumu kukabiliana na uhamiaji usio halali, la muhimu waweze kufika nchi za Ulaya hasa nchini Ufaransa na Italia. Mtafiti mmoja Luciana De Michela anabainisha kwamba uhamiaji usio halali umetokana zaidi na ubalozi kuwanyima visa ya kuingilia nchi za Ulaya kihalali. Aidha anasema, zamani ilikuwa ni rahisi kuwajongea ndugu zao kama baba au kaka zao kwa ajili ya kuweza kusaidia ndugu kiuchumi bila kupitia zenye mikato na hatari lakini kwa sasa  imekuwa vugumu , ndiyo maana vijana wengi wanaamua kuanza safari ya hatari kuliko kubaki katika nchi yao ya Senegal ambayo haiwasaidii vijana wake katika ajira au masomo.

Halikadhalika Madhimisho ya Siku ya Afrika yamefanyika hata katika maeneo mengi hata  nchi kama vile  Uturuki, kwani  wizara ya mambo ya nje ya Uturuki ilifahamisha kuwa serikali ya Ankara itazidi kuimarisha ushirikino wake katika Nyanja tofauti na mataifa ya bara la Afrika. Tangazo lililotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Uturuki  limefahamisha kuwa ni kwa heshima kubwa Uturuki inaadhimisha siku ya Afrika kuonesha ushirikiano na kuwa na nia ya kuzidi kuhimarisha ushirikiano na mataifa ya bara la Afrika katika nyanja tofauti. Serikali ya Uturuki imesema kuwa itaongeza juhudi zake katika kuimarisha ushirikiano uliopo baina yake na bara la Afrika.

Wizara ya mambo ya nje ilikumbusha kuwa Siku ya Afrika ni ajili ya kuadhimisha kuundwa kwa Umoja wa Afrika tangu mwaka 1963. Umoja wa Afrika uliundwa Mei  25 mwaka 1963. Halikadhali tamasha kuhusu siku ya Afrika nchini Uturuki huandaliwa maonesho ya kitamaduni yanayowakilisha nchi za bara la Afrika na Mke wa rais wa Uturuki Bi Emine Erdoğan alikuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo.Tamasha hilo la kitamaduni liliandaliwa katika chuo kikuu cha Gazi mjini Ankara.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.