2017-05-23 14:42:00

Madagascar: Maaskofu wanashutumu vikali mauaji katika maeneo ya nchi


Mbele ya hali mbaya inayoikabili  nchi katika nyanja mbalimbali , Baraza la Maaskofu  Katoliki wa Madagascar hivi karibuni wamechapisha ujumbe wao unaowalenga wabatizwa wote na watu wote wenye mapenzi mema wakiwakuwakumbusha  aya ya  Injli ya Mtakatifu Luka isemayo “ basi onyesheni kwa vitendo kwamba mmetubu” (Lk 3,8). Barua illiyotolewa hata katika Shirika la Habari Katoliki la Fides, inaanza na kushutumu vikali mauaji ambayo yamejitokeza katika maeneo tofauti ya nchi ya Madagascar kama vile Antsakabary, Antsirabe na Antsohihy. Maaskofu  hawaridhiki tu na  uelewa wa dhamiri  bali wanatoa wito kwa wote kuwa na uongofu wa kweli ili mabadiliko ya kweli yaweze kuonekana.

Kwa namna hiyo maaskofu wanawaalika wazelendo wote  wawe uongofu wa kweli kwa kuiga mfano wa Baba Ramose Lucien Botovasoa, aliyekuwa mlei na Mfransiskani wa utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko  na baba wa familia , aliye uwawa huko Vohipeno (Madagascar kwa ajili ya kutetea imani yake tarehe 17 Aprili 1947.Ni mmoja wa wale ambao Baba Matakatifu  Francisko tarehe 4 Mei 2017 ameweza kumweka katika orodha ya mashahidi wa kutangazwa watakatifu. Baba huyo Botavasoa ameelezwa kuwa ni shahidi wa imani na upendo , alikuwa ni mtu mwongofu, asiyekuwa na uharibifu wa maisha na shahidi wa ukweli na maridhiano, ambaye alitoa maisha yake kwa taifa akisema “damu yangu inayomwagika iweze kusaidia ulinzi wa nchi yangu.”

Katika ujumbe wao Maaskofu pia wanaalika mamlaka ya Kanisa kutafakari kwa kina juu ya kupambana na udhaifu ambao unaleta kashfa aidha kutoa tahadhali kwa wahusika wa maisha ya umma hasa katika  sekta zinazohusu afya , elimu na mafunzo, usalama wa umma na ulinzi wa taifa. Maaskofu pia wanakumbusha majukumu ya kila mmoja anayopaswa kuwa nayo kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli. Na mwisho wanaalika watu wote kufanya maombi  hasa  novena kuanzia siku ya kupaa kwa Bwana hadi kufika jumamosi ya mkesha wa ujio wa Roho Mtakatifu Pentekoste.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.