2017-05-22 14:11:00

Kard. Filoni: Kila mbatizwa atoe ushuhuda wa kutangaza Yesu mfufuka


Mkinipenda na kuzishika amri zangu. Sitawaacha yatima , nitakuja kwenu, ni maneno ya Yesu aliyo tamka kwa mitume wake kabla  ya kifo na kurudi kwa Baba yake. Ni maneno ambayo hata leo yanatoa mwangwi katika Kanisa hili ambalo linapewa wadhifa wa Kanisa Kuu la Evinayong.
Ni maneno ya utangulizi wa mahubiri yake Kardinalai Fernando  Filoni, Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu  katika Ibada ya Misa kuu ya kisimkwa Rasmi, Askofu Mpya  Katika Jimbo Jipya  nchini Equatorial Guinea Jumapili ya tarehe 21 Mei 2017.
Kardinali F Filoni ambaye yuko hija ya kitume katika nchi ya Equatorial Guinea kwa ajili ya tukio la kutoa wakfu wa Maaskofu watatu, ambao tukio hilo lilikuwa Jumamosi 20 Mei 2017, katika mahubiri haya anatafakari upendo na amri ya Mungu kutoka katika Injili ya Jumapili ya sita ya pasaka. Anasema wameunganika pamoja kwa uhakika kwamba Bwana amefufuka , ni mzima  na yupo kati ya wote, kama alivyo toa ahadi ya kwamba  mimi sitawwacha yatima , bali nitakuja kwenu (Yh 14,18). Uwepo wake kati yetu siyo tu sababu ya kutulizwa bali zaidi ni uaminifu wake  wa kutia moyo ya kwamba sisi hatuko peke yetu na wala siyo yatima.

Kardinali Filoni amewakilisha salam na baraka za kitume kutoka kwa  Baba Mtakatifu na kusema kwamba Kanisa la Equatorial Guine liko rohoni mwake, hadi kufikia kuunda Jimbo jpya la Evinayong na Mongomo; Ambapo  amekumbusha juu ya kuwaweka wakfu maaskofu watatu katika moja wapo ya Jimbo jipya Mongomo na kwamba wamepata furaha kubwa kwa tendo hilo la kuwekwa wakfu dugu maakofu watatu. Anarudia kumtakia Askofu Mpya Callixto –Paulino utume mwema wa kiaskofu pia kwa waamini wote katika safari ya Kanisa Katoliki la Equatorial Guinea , lenye kuwa na utambuzi wa utume wake  kati ya wazalendo  wenye mapenzi mema ya nchi.Aidha ametoa  salam kwa mapadre, watawa wote akiwatia moyo , ya kwamba watambue utume wao unao wataka wajitoe bila kubakiza kati ya matatizo ya kila aina:; kwenu ninyi anasema, imeanzishwa  mshikamano wa kuunda Jimbo ambalo ni Familia ya Kanisa , kwa njia hiyo ametaka matashi mema ya neema ili ishuke kati yao na amani kutoka kwa Mungu Baba wa Yesu Kristo  ” (1 Co 1,3).

Katika somo la kwanza kutoka  masomo ya Jumapili ya sita baada ya Pasaka anasema linakumbusha kwamba Kanisa limezaliwa kwa ajili ya kuinjilisha. Hiyo ni wazi kutokana na kwamba Yesu aliwachagua mitume wake ili wawe mashuhuda wa ufufuko. Ni kwa njia ya  madaraja hayo ya kuweza kusambaza habari ya ufufuko ambayo ilianza kutangazwa na mitume waliokabidhiwa  utume huo na Yesu mwenyewe. Kwa maana hiyo hata Shemasi Filipo katika mji wa Samaria alikwenda kuwahubiri kuhusu Kristo aliyekufa na kufufuka.Tangu wakati huo Kanisa linaendelea kufanya utume wenyewe, ambao unajikita kwa wabatizwa wote ili kuwajibika bila kuchoka daima. Kumtangaza Kristo ni utume ambao Kanisa daima ni lazima kufanya kwa kila yoyote mbatizwa bila kuchoka amesisitiza Kardinali Filoni.

Kama alivyo fanya mtakatifu Filipo huko Samaria enzi zile , ndivyo ilivyokuwa miaka ya 1645 ndugu wafransiskani Wakapuchini wa kwanza walifika Equatorial Guinea ya sasa. Hawa kama wamisionari wengine waliofuatia , padri wa Jimbo la Toledo, Wayesuiti na zaidi Waklaretiani, walihubiri Yesu katika ardhi hii na kuonesha ushuhuda kwa waamini. Walijibidisha kuwaonesha ndugu wa nchi hii njia ya wokovu na kumtangaza Yesu. Kwa namna hiyo wao na ninyi mlio hapa, nina watolea shukrani na utambuzi wa utume wa   uinjilishaji walioufanya kwa kuweka msingi wa Kanisa kati yenu, na kwa namna hiyo hakuna mtu mwingine aweza kuweka msingi tofauti na huo.Kwa dhati ndiyo msingi huo ambao leo hii umewekwa na ndiyo  nyumba ya kiroho, yaani jumuiya mpya ya Kanisa la Evinayong  ambao una fungua ukurasa mpya wa Kanisa la Equatorial Guine.Kardinali Filoni anatoa mfano mmoja ya kwamba mtoto anapozaliwa katika familia, swali la kwanza ni kujiliza , je atakuwaje ? kwa maana ya hali halisi ya Jimbo jipya la Vinayong litakuwaje?  (Lk 1,66).

Lakini amesema, swali kama hili linaeleza wakati huo huo wasiwasi mkubwa na pia matumaini hai. Wasiwasi na matumaini hayo yanajieleza zaidi katika matashi ya kuishi ndani ya mioyo ya wote, kwa maana ya kuona wamba, Jimbo jipya la Evinayong linakua na kuwa na utajiri wa Kanisa lote kwa nguvu hai. Aidha wasi wasi huo na matumaini pia yapo katika Jumuiya yote ya kikristo ya Guinea Equtorial baada ya kuundwa ndani yake Jimbo jipya. Kanisa Katoliki la Guinea , kama kila familia, matarajio yake ni kuona Jimbo jipya la Evinayon linakua na pia kuwa na ukarimu wa maendeleo, utajiri wa kiroho na zaidi kujitoa kwa nguvu zote katika uinjilishaji. Kwa hakika ni kwamba Jimbo jipya halitaachwa peke yake kwasababu Bwana Yesu anatoa uhakika wa uwepo wake daima kwa maneno haya” sitawaacha yatima”.Tendo la kusikia uhakika wa kutokuachwa peke, ni kitulizo mbele ya hatari ya matatizo makubwa,maeneo   haya yanaleta uhakika wa kufanya uzoefu wa kitulizo, kupokelewa na kusindikizwa mbele ya matumaini ili kuweza kukua na kushi.
Kardinali Filoni anaendelea kusema,  jimbo jipya linaitwa kutoa  matumaini haya ya kuweza kuishi na kukua, lakini limekabidhiwa ili litunzwe. Kwa namna hiyo inategemea na ninyi kama mtoto mchanga ategemeavyo mama yake. Kama mbegu ndogo , jimbo jipya limekabidhiwa kama vile wanyakazi katika mashuhuri katika shamba . Wanaalikwa kutunza ili kuwa mti mkubwa ambao unaweza kutoa matunda, kama Yesu alivyotoa mfano wa mbegu ya aladali, baadaye ikakua, ikawa mti mkubwa kiasi cha ndege wa hangani kufaidi matunda ya mti huo.

Wamisionari waliopitia wamepanda Neno la Mungu , na sasa ni ninyi mpaswa kumwagilia shamba ili mbegu ziweze kuota vizuri. Kwa njia hiyo wahusika wote wa Kanisa wanachangia kukuza mti huo ambo ni Jimbo la Evinayong. Kardinali Filoni anaonya kwamba “Msipande magugu mabaya katika shamba la Bwana, kwa maana ya kwamba wasipande vurugu, chuki, wivu na masingenyo.
Aidha wamieitwa kuwa wajenzi wa Kanisa, lililojengwa hawali ya yote na Kristo msingi usio haribika.Na kila mmoja awe makini katika ujenzi na busara ya mjenzi, ambayo Mtakatifu Paulo anafundisha. Wadumishe ujenzi wa Kanisa kwa njia ya tunu ya upendo wa kindugu, ushirikiano na umoja: watumie mawe athamani kama vile ya uhuruma, mshikamano, ukweli na haki, wasizue migongano na wala mafao binafsi , kama vil dhambi ya ulaghai.Wawe makini kwasababu Yesu aweze kukubalika kati yao na kukuta furaha ndani ya nyumba yake.

Katika kazi ya ujenzi wa Jimbo wote ni wahudumu wa Mungu, kiukweli mjenzi wa Kanisa ni  Mungu mwenyewe ambayehukuza mbengu hiyo. Ndiye anayepaswa kuabudiwa katika mioyo ili kuwa tayari kujibu maswali ya sababu ya imani na matumaini ya kikristo. Ahadi ya Bwana ya kwamba nitakuja kwenu, ni uhakika ya kwamba tusiwe na hofu kwasababu Bwana Yesu mwenyewe anatimiza ahadi yake siku zote hadi mwisho wa dunia.(Mt 28,20)
Mkinipenda na kuzishika  amri zangu, kwa mujibu wa Injili ya MtakatifuYohane ni kutaka kuonesha kwamba siri ya mambo yote ni upendo wa Kristo.Utume wetu wa kikristo na wa Kanisa unatokana na msingi wa upendo, la sivyo inageuka kuwa za shughuli kijamii. Kila aina ya utume na kila aina ya shughuli za kimisionari. Huduma ya Kanisa ina msingi wa upendo wa Kristo ambayo ndiyo inapswa kupewa kipaumbel.Ni lazima kukumbuka maswali matatu ya Yesu aliyo muuliza; "Simoni wa Yohane wanipenda", "Simoni wa Yohane wanipenda zaidi ya chochote", "Simoni wa Yohane wanipenda kweli?
Majibu ya Petro yalikuwa ni yenye ukarimu na ukweli kwasababu alijibu: "Bwana wewe wajua yote, wajua nikupendavyo".Upendo huo wa Kristo unatokana na kazi ya kitumeambayo ni "kuchunga kondoo” (Yh 21,16.17).

Kila tendo la Mkristo na uchungaji una msingi wake wa upendo kwa Bwana, Utume wa Kanisa unaelekeza upendo na kujitoa sadaka: kwa njia hiyo utume wa Kanisa unajieleza hawali ya yote katokana na ushuhuda kwa Kristo, Mwalimu na Bwana. Kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko: Ushuhuda wa Kristo ni njia mwalimu ya uinjilishaji. Mfano wa upendo wa Mungu aliyejionesha kwetu sisi kwa njia ya mwanae mzawa wa kwanza (1Yh 4,9),hata upendo wa mkristo kwa ajili ya Bwana lazima uwe wa ukarimu na kujitoa kabisa.
Mwisho Kardinali Filoni anasema maneno hayo ya Yesu mwaliko  wa kuishi daima wito wetu wa dhati kwa Kanisa ambalo ni fumbo, kwa namna hiyo ni kutoa ushuhuda wa kijasiri wa Injili,katika kupeleka matumaini kwa masikini, wanaoteseka, waliobaguliwa na wanye kuteseka, hata wenye kiu ya upendo, uhuru ,ukweli na amani.

Sr Angela rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.