2017-05-19 16:45:00

Papa: Roho ya Mungu inaunganisha Kanisa, itikadi zinagawa Kanisa


Mafundisho ya kweli unganisha kinyume na itikadi ugawanya, ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha Mjini Vatican asubuhi tarehe 19 Mei 2017 akitafakari juu ya msemo wa mtaguso wa Yerusalem kati ya miaka 49 baada ya Kristo,kuhusu namna gani ya kutoa  maamuzi ya wapagani walio kuwa wanataka kubadili kuwa wakristo bila kutahiriwa kwa mujibu wa sheria ya musa ilivyokuwa ikisema .Akitafakari juu ya somo la kwanza kutoka katika  matendo ya mitume , Baba Mtakatifu anabaisha kwamba hata katika jumuiya  ya kwanza ya kikristo kati yao kulikuwa na wivu, mapambano ya madaraka na ujanja wa kutaka kununua madaraka. Kwa namna hiyo anasema, daima kumekuwa na matatizo: sisi ni binadamu na wadhambi, na matatizo yapo hata katika Kanisa, lakini uelewa  kuwa sisi ni wadhambi linatufanya kuwa wanyenyekevu na kumkaribia Bwana kama mwokozi wa dhambi zetu.

Kwa upande wa wapagani ambao Roho Mtakatifu alikuwa amewaita wawe wakristo,  Baba Mtakatifu anakumbusha neno lilisomwa kwamba mitume na wazee walichagua kati yao kwenda Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Haya ni makundi ya watu yanayoelezwa kwamba sehemu moja ilikuwa yenye madadiliano ya nguvu na nyenye roho nzuri , na sehemu nyingine yenye kuchanganya.
Kwa maana hiyo , kulikuwa na kundi la mitume wanaopenda kujadili matatizo na wengine wanaopenda kufanya matatizo na wanatenganisha kwasababu , walikuwa wakitengenisha Kanisa kutokana na kusema kuwa  mitume walikuwa wanahubiri mambo ambayo hakusema Yesu .Lakini hakuwa kweli ,Kwasababu mitume walichojadili kati yao mwisho wake walifikia uamuzi.

Baba Mtakatifu anaendelea kusema  walifikia makubaliano kwasababu hayakuwa majadiliano ya kisiasa , bali yalikuwa majadiliano kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye aliwafikisha hatua ya kusema kuna jambo na hakuna mahitaji. Majadiliano hayo yallikuwa yakihusu kula nyama ambayo imetolewa kafala lwa miungu, kwa maana ilikuwa ni kula nyama  ya miungu na kushibishwa damu ya wanyama walio chinjwa kihalifu
Baba Mtakatifu Francisko amebainisha na kuonesha uhuru wa Roho ambayo uleta makubaliano, na mwisho wapagani kuweza kuwa sehemu ya Kanisa bila kipitia sheria ya kutahiriwa. Kwa njia hiyo ndiyo ikaanza Mtaguso wa kwanza wa Kanisa , maana ni Roho Mtakatifu yaani Papa na maaskofu wake pamoja, waliounganika kuweka wazi mafundisho , ambayo yamefuatwa kwa mihongo mimgi, kama vile ule  wa Mtaguso wa Efeso na  wa Vatican II; Baba Mtakatifu anabainsha kuwa hiyo ni kwasababu ya ulazima wa Kanisa kuweka wazi mafundisho ili kuweza kuelewa vema Yesu alisema nini katoka katika Injili na  Injili zote zina roho gani.

Hata hivyo Baba Mtakatifu anaonesha kwamba daima kumekuwapo watu ambao bila hata ya kutumwa , wamekwenda mara nyingi  kutoa usumbufu katika jumuiya za kikristo kwa maneo ya kushtusha,kwa mfano huyo kasema hivi amemkana Mungu , au haya siyo mafundisho ya Kanisa. Au wengine kwenda kupanda begu mbaya ya kutengenisha jumuiya za Kikisto. Haya ni matatizo hasa inapojitokeza mchanganuo  kati haya ni mafundisho ya Kanisa, haya yanatokana na Injili, haya yametokana na roho Mtakatifu  au kwasababu Yesu mwenyewe alisema, yeye atakaye fundisha na kuwakumbusha yale ambayo aliyofundisha. Kwa njia hiyo baba Mtakatifu anaonya kwamba ni kuleta mchanganyiko kwa watu.
Kwa maana Roho Mtakatifu anaunganisha na siyo kutengenisha, kwa aana hiyo enzi hizi watu hao hawakuwa na waamini bali walikuwa ni wenye itakadi ambazo zilifunga mioyo yao kwa roho Mtakatifu.

Lakini mitume hao wakwa hakikia walijadiliana nao lakini hakuwa na itikadi , walikuwa wazi miyo yao na kusikiliza roho Mtakatifu anasema nini. Na baada ya majadiliano Roho mataktifu alito ana kuwaeleza wasiogope mbele ya vitishio na mawzao ya itikadi za mafundisho hayo.
Kwa njia hiyo Baba Mtaktifu Francisko anamalizia akisema Kanisa lina utu,e wake kwa njia ya Papa , amaskofu na mitaguso, ambapo tunalazimka kutembe akatika njia hiyo, inayotokana na mahubiri ya Yes una mafundisho kwa njia ya roho mtakatifu, abaye daima ni wazi , na kwasababu mafundisho ya Kanisa yanaunganisha , na mitaguso inaunganisha jumuiya ya kikristo bali itikadi zinagawanya.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.