2017-05-17 16:40:00

Papa kutembelea Parokia ya Mt. Pier Damiani, Roma, tarehe 21 Mei 2017


Baba Mtakatifu Francisko Jumapili tarehe 21 Mei 2017 anatarajiwa kutembelea Parokia ya Mtakatifu Pier Damiani Roma Italia. Huko atapokelewa na Kardinali Agostino Vallini Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Roma na ambaye Kanisa hilo ambalo ndilo alikabidhiwa wakati wa kusimikwa kuwa Kardinali, pia  askofu Msaidizi wa Roma ya Kusini Paolo Lodjudice, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Pier Damiani na wahudumu Parokia . Wakati wa ziara yake hiyo atakutana na vijana, wagonjwa, familia na watoto waliobatizwa mwaka huu na wahudumu wa kichungaji wa Parokia , aidha ataungamisha watu wanne na kuadhimisha ibada ya misa saa 12 Jioni.

Hiii takuwa ni ziara yake 15 ya kichungaji katika parokia za Jimbo lake Kuu. Baba Mtakatifu Francisko atakuwa papa wa tatu kutembelea jumuiya ya parokia hii wa kwanza alikuwa ni Mwenye heri Paulo VI mwezi Februrari 1972 wakati wa kuadhimisha jubilei ya miaka 100 ya kifo cha Mtakatifu Pier Damiani, na Mtakatifu Yohane Paulo II aliyetembelea Parokia hiyo tarehe 13 Machi 1988. Baba Mtakatifu kabla ya Misa hiyo atakutana na watoto wa 80 wanaoudhuria katekisimu wakiwa katika maandalizi ya kupata komunio ya kwanza,pia zaidi ya vijana 100 wanaoudhuria mafunzo ya kipaimara. Baadaye anatafanya mkutano na watu wagonjwa , wazee , familia na watoto wao waliobatizwa mwaka huu, pia wanachama wa Chama cha Wakatekumeni, wahudumu wa kichungaji pamoja na watu wa kujitolea wa Caritas, watu wanne wanatarajiwa kuungamishwa na Baba Mtakatifu Francisko.

Jumuiya  ya Parokia ya Mtakatifu Pier Damiani inayo furaha ya kumpokea Baba Mtakatifu Francisko, kwani hayo yamesemwa na Padre Lucio Paroko wa Parokia hiyo ambaye ni Paroko tangu mwaka 2005. Akielezea juu ya Parokia  iliyoko pembeni Kusini mwa Roma kwamba kuna uhaba wa huduma muhimu  kama vile huduma za masoko makuu, au kazi kuwa mbali,ambapo watu wanalazimika kuamka mapema sana kuwahi usafiri ili kufikia maeneo ya kazi pia wanarudi usiku. Pamoja na kwamba siyo wote wanaojihusisha kuudhuria ibada za kila siku, lakini wanajitahidi kutoa michango  iwapo inahitajika na kutoa huduma mbalimbali za Parokia , kama vile Caritas, na vitengo vyake vya huduma za kijamii katika parokia hiyo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.