2017-05-16 16:03:00

Papa akutana na Timu ya Mpira ya Juventus na Lazio nchini Italia


Jumanne tarehe 16 Mei 20 17 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na viongozi wa Kitaifa na wanamichezo wa timu ya mpira wa miguu Juventus na Lazio mjini Vatican, wakiwa wanajiandaa  na michuano ya kuwania mshindi wa kombe la Italia. Baba Mtakatifu anasema kuwa anayo furaha ya kuwapokea na kumshukuru Rais wa Shirikisho la vyama vya Mchezo wa Mpira  kwa maneno ya hotuba yake aliyoitoa na  kuwapongeza timu zote mbili Juventus na Lazio na kusema, pamoja na matokeo mazuri waliyo nayo kimichezo kama washindi bado wanapendwa na washabiki wengi. Hivyo ina maana kuwajibika na kutoa ushuhuda wa dhati kuonesha thamani ya michezo.

Aidha amesema anataka kurudia  mada kwa ufupi inayohusu umuhimu na thamani ya michezo kwa nyakati zetu. Kwa kufikiria jinsi wanavyo pendwa, na jinsi gani wao ni wataalam ambao wanabeba uwajibu huo mabegani mwao. Zaidi wao ni vijana ambao wana majukumu makubwa sana; maana  anasema, wao wanafikiriwa ni washindi (Champion) ambapo wanazo sifa za kuigwa mifano. Baba Mtakatifu anaongeza akisema , kwa njia hiyo kila aina ya mchuano ni jaribio la uwiano wa kujiaminisha na kuheshimu sheria. Yeyote anayejua tabia yake na kuweza kukubali majaribu na kutoa ushuhuda huo, anageuka kuwa mfano bora kwa watazamaji na wapenzi wake. Hayo ndiyo matashi mema anayo watakia kwamba,wawe mashuhuda halisi, waaminifu , wakweli , wapatanishi na kuwa na ubinadamu.

Baba Mtakatifu amesema wakati mwingine kwa bahati mbaya katika viwanja vya mpira yapo matukio ya vurugu ambayo husababisha na  kuharibu utendaji wa amani mahali ambapo watu wanaburudika. Ni matumaini ya kwamba kwa nguvu ya uwezo wao wanaweza kusaidia michezo ibaki jinsi ilivyo, hiyo ni pamoja na shukrani za juhudi ya dhamira binafsi kwa wote ili kuwa chanzo cha mshikamano kati ya wanamichezo na jamii nzima.

Amemalizia Baba Mtakatifu Francisko akiwashukuru kwa moyo wote kufika kwao kumtembelea na kuwatakia wafanye kweli mchezo mzuri. Na kuwapatia baraka wote hata familia na  wapendwa wao, Bila kusahau kuwaeleza wasali kwa ajili yake.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.