2017-05-16 15:39:00

Amani ya ndani ni zawadi kutoka katika vipawa vya roho Mtakatifu


Amani ya kweli haiwezekani kuitengeza katika viwanda vyetu sisi wenyewe, ni zawadi ya Roho Mtakatifu. Amani bila kuwa na msalaba siyo amani ya Yesu kwa maana ni Bwana peke yake mwenye uwezo wa kutupatia amani mbele ya majaribu na mateso. Ni maeno kutoka katika mahubiri yake Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Mei 2017 wakati wa Ibada ya misa Takatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha Mjini Vatican. Ninawapa amani na kuwaachia amani, ni maneno ya Yesu aliyoyaseama wakati wa Kalamu ya mwisho akiwa na mitume wake.  Baba Mtakatifu akiongozwa na maneno hayo anatoa maana ya amani aliyoitoa Bwana Yesu akiwa na mitume wake. Katika somo la siku kutoka kitabu cha matendo ya mitume, somo linaeleezea juu ya majaribu mengi waliyoyapata Paulo na Barnaba katika safari yao ya kutangaza Injili. Baba Mtakatifu anauliza, je hiyo ndiyo amani aliyotoa Yesu? Kwa kuchambua zaidi anasema, Yesu anasisitiza kuwa amani anayowapatia siyo itokayo ulimwengu huu.

Kwasababu amani inayotolewa na ulimwengu, ni ile isiyo kuwa na majaribu, ni amani isiyo ya kweli , amani  ya utulivu wa bandia. Kwa maana ni amani inayotazama mambo binafsi , usalama binafsi ya kwamba usikosena kupungukiwa lolote; anaongeza Baba Mtakatifu akisema ; ni kama ile amani ya tajiri na masikini Lazzaro. Huo ni utulivu wa bandia unaokufanya kujifunga binafsi bila kutazama upeo zaidi. Baba Mtakatifu anafafanua zaidi kwa kutua mifano halisi; dunia inatufundisha  njia ya amani ambayo imepigwa sindano ya usingizi, kwani ukiwa umepigwa sindano ya dawa ya usingizi inakufanya usitazame hali halisi ya maisha hasa msalaba. Kwa njia hiyo ndiyo maana Paulo anasema ni lazima kuingia katika ufalme wa mbingu ukitembea katika majaribu. Je inawezakana ukawa na amani wakati uko katika majaribu? Anatoa swali Baba Mtakatifu Francisko na kusema , kwa upande wetu haiwezekani kwasababu hatuna uwezo wa kufanya amani yenye utulivu, au amani ya kisaikolijia, amani inayotengenezwa na sisi wenyewe, kwasababu kuna mateso, zipo shida, badhi ni wagonjwa na pia vifo na vita, kwa njia hiyo majaribu yapo.

Lakini amani anayoitoa Yesu ni zawadi, ni vipawa vya Roho Mtakatifu, ni amani katikati ya majaribu na inapiga hatua mbele zaidi. Aidha anaeleza;  hiyo siyo aina ya hali ya kutokujali furaha wala huzuni wala maumivu, kama ile afanyavyo mchukuzi, hii ina maana nyingine,amesisitiza.
Amani aitokayo Mungu ndiyo inatufanya tuendelee mbele. Yesu baada ya kuwapa amani mitume wake, aliteseka katika shamba la mizeituni, pale alitoa utashi wake Baba na kuteseka, lakini hakukosa kitulizo kutoka kwake  Mungu kwasababu, Injili inaeleza kwamba alitokea Malaika kutoka mbinguni kumtuliza. Amani itokayo kwa Mungu ni ya dhati, ambayo inajikiti katika maisha halisi na wala haikanushi maisha maana maisha ndivyo yalivyo, yapo mateso , magojwa na mambo mengi mabaya na kuna vita.  Lakini amani ya ndani ni zawadi, ambapo amani hiyo huwezi kamwe kuipoteza  maana inatoa msukumo wa kwenda mbele na kubeba msalaba na mateso. Amani bila msalaba siyo amani ya Yesu, ni amani ambayo unaweza kuinunua na  kuitengeneza mwenyewe binafsi, lakini haitadumu kamwe itakwisha.

Aidha Baba Mtakatifu anatoa mfano, iwapo mtu anachukia hupoteza amani, iwapo moyo unasononeka unakosa amani kwasababu ya kufunga amani itokayo kwake Yesu; huo ni ukosefu wa uwezo wa kupokea maisha jinsi yanavyojitokeza ya misalaba na mateso yake. Kwa njia hiyo Baba Mtaktifu Francisko anatoa ushauri kuwa ni lazima kuwa na uwezo wa kuomba neema kwa Bwana ili kuwa amani. Amemalizia akisema, tunapaswa kuingia katika ufalme wa Mbingu kwa kupitia  mateso mengi na neema ya amani isipoteze amani ya ndani, kama vile Mtakatifu mmoja alivyosema kuwa, Maisha ya Mkristo ni safari kati ya mateso ya ulimwengu huu na faraja kutoka kwa Mungu (Taz: Mt.Agostino ,Dei XVIII,51); hivyo Bwana atufanye kuwa utambuzi mwema  juu ya amani itokayo kwake ni zawadi ya Roho Mtakatifu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.