2017-05-15 13:11:00

Vijana salini Rosari ili kupata ujasiri na nguvu katika maisha!


Inabidi kugundua kwa upya uwepo wa Maria katika maisha na kama mfano na msaada wa uchaguzi wetu. Ni matashi mema aliyoyatoa Kardinali Agostino Vallini Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Roma alio watakiwa vijana wengi walioudhuria mkesha wa Mama Maria katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuuwakiungana na mkesha wa mama Maria mama yetu huko Fatima. Mkesha huo uliandaliwa na huduma ya kichungaji ya Vyuo Vikuu kijimbo kwa ushirikiano wa Huduma ya kichungaji kwa  vijana na miito katika tukio la maadhimisho ya miaka 100 ya kutokea Mama yetu wa Fatima. Maandalizi ya mkesha kwa vijana yamekuwa sambamba  pande za dunia, kuanzia Roma, Fatima ,Buenos Aires, Czestochowa na Nazaret na nyinginezo. Ni hatua ya sala ya Maria kwa vijana iliyo andaliwa  kusali Rosari wakiungunika moja kwa moja katika madhabahu makuu manne. Ni sura ya Maria kwa njia ya kusali matendo ya furaha ambayo yamewasindikiza katika safari hiyo kuelekea mahali ambapo Maria mwenyewe Maria alijionesha.

Kardinali Valini aliye ongoza mkesha huo amesema; ni kufunga siku ya imani kubwa kwa Mama Maria mama yetu na  mama wa dunia nima. Kwani kutoke Fatima, tumesikia moyo wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko, katika madhabahu ya Roma yanayowakilisha  ulimwengu yaani katutoka madhabahu ya Maria Mkuu , mahali ambapo Baba Mtakatifu kabla ya kwenda au baada ya kurudi anakuja katika Kanisa hili kuomba na kutoa shukrani. Tumetoa sifa na kuomba kwake Mama Maria kwa njia ya matendo ya rosari ya furaha, kumwomba nguvu mama yetu ili tusiachae kamwe  kumkibilia katika maisha yetu na zaidi aangaze maisha yetu na kutupatia nguvu,ujasiri na furaha. Kwa njia hiyo tunaweza kusema tunayo furaha ya siku ya leo kwa neema zake Bwana anazotujalia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.