2017-05-15 12:51:00

Kard. Sandri katika Ziara yake ya Kitume nchini Australia!


Tarehe 14 Mei 2017 Kardinali Leonardo Sandri ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Watakatifu Petro na Paulo  huko Melbourne akiwa na Askofu Peter Stasiuk, Balozi wa Papa  huko Australia Askofu Mkuu Adolfo Tito Yllana, Askofu Mkaladayo Nona pia wa Kimaroniti Tarabaye na mapadri wote.  Akiongozwa na Neno la Mungu wakati wa kipindi hiki cha Pasaka, amewashirikisha kwa nguvu zote juu ya kuwa na matumaini.

Baada ya misa chakula cha mchana amekuwa na Jumuiya ya watawa kutoka Brazil wakiwa wanaadhimisha mwaka huu miaka 50 ya uwepo wao katika nchi ya Australia. Mchana Kardinali aliondoka na maakofu waliotajwa hapo juu  kwendaa kwa  Askofu wa Wamelkti Askofu Robert Rabbat na Msaidizi wa Kipatriaki Katoliki wa Romania huko Astralia askofu Sosanian  Kaskazini mwa Melbourne. Ambapo katika kiwanja cha  mpira cha chuo cha Mtakatifu Yohane ,mahali ambapo ameadhimisha liturujia na sala  wakiwa na Askofu  Bosco Puthur wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Thamas wa Syro-Malabar huko Melbourne, aliyechaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko Desemba 2013.

Uwanja huo ulifurika watu wengi wakiwa ni familia vijana na watoto wao wengi, waliokuwa wamevalia nguo zao za  kiutamaduni wa India, waliimba nyimbo katika lugha ya Kerala na Malyalam. Ni jambo la kufurahisha kuona watu rahisi na furaha inayaoambukiza watu wote katika kuimarisha mizizi yao ya kikristo ambapo kwa sasa bado hawajawa na Kanisa lao kuu lakini kwa wako katika mchakato wa kupeleka mbele mipango ya eneo linalofaa ambalo wamenunua  japokuwa wanacheleweshwa na ukiritimba wa ruhusa muhimu kutoka kwa serikali kwa ajili ya kuanza kazi.
Mapadre wa Malabaresi walioshiriki maadhimisho hayo walikuwa 30 ambao wanatoa huduma katika majimbo  hayo , mapadre hawa wanatumwa na maaskofu kutoka India ili waweze kusaidia waamini wa majimbo hayo wakisaidiana pia na mapadre kutoka Amerika ya Kusini ambapo inasaidikiwa kuwapo waamini 4000,000 kutoka katika Kanisa la Siro Malabarese nchini India wanaishi huko Australia.

Baada ya madhimisho matakatifu na kuvua nguo za ibada walishiriki wote kutazama piacha  picha ya kuonesha historia ya uwepo wa waamini kutoka Malabaresi walioko nchini Austaria.Zilitolewa pia hotuba mbalimbali za shukrani , kati ya hizo ni ile ya Balozi wa Kipapa nchini Australia Askofu Mkuu Adolfo Tito Yllana, kutokana na uwepo wa familia nyingi vijana na watoto wengi amewashukuru kwa ushuhuda wao, na kuwatakia matashi mema wakina mama kutokana na tukio la Siku ya Mama duniani , akirudia wimbo wa ("I am, You are, We are Australians"), mimi, wewe, sisi ni waustralia.

Amewakumbusha kwamba watu walio wengi sasa ni wazalendo wa Australia , wengi wao wana ruhusa ya moja kwa moja ya kuishi nchini Austalia , ambapo wanaweza kusema sisi ni wa Australia , lakini bila kupoteza furaha ya kuwa wakatoliki  kwa mujibu wa utamaduni wao wa  Siro- Malabarese, na kuunda Kanisa moja katoliki katika jamii ya Australia pamoja na ndugu wote wa Amerika ya Kusini, wakaldayo, Mronite , melkiti , Ucrain Arimeina na wakopti wanaoishi Australia. Chakula cha jioni Kardinali Sandri alishiriki na baadhi ya mapadre mahalia wanaoishi katika eneo lenye mkakati wa ujenzi wa Kanisa Kuu kabla ya kuondoka kurudi Sydney.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.