Katika mji wa Amman, nchini Jordania, umezinduliwa mtandao wa kudumu kati ya Taasisi na vituo vya mafunzo ya elimu ya juu katika vyo vikuu vya Kiislam na wahudumu wakristo wanaosoma au kufanya kazi katika nchi za Uarabuni. Hayo yamefanyika wakati wa Mkutano katika kituo cha Kimataifa cha mazungumzo cha Kaiciid na Diyar Constortium hivi karibuni. Jukumu muhimu la Taasisi za Elimu ya Juu yenye asili ya dini katika maisha ya kila siku ni kupinga juu ya kuchakachua masuala ya kiteolojia na Mafundisho ambayo kwa muda mrefu viongozi wa kisiasa wamekuwa wakialikwa kuchambua na kutafuta mbinu na hatua ambazo wangeweza kujiuliza jinsi ya kuondokana na migogoro ya kidini ambayo ndiyo mama wa marumbano y amara kwa mara katika bchi hizo.
Onyo hilo pia limetolewa hata kwa upande vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
ambayo mara nyingi imekuwa ikikanusha ukweli huo na kutofuata wito, lakini ki ukweli
ndiyo asili ya kufanya kampeni za kuchochea chuki za kidini ambazo uongeza vurugu
na vita vya kidini.
Kwa njia ya kuweka mikakati ya ushirikiano, wa vituo vya Diyar na Kaiciid wameunganisha
wawakilishi kutoka katika taasisi za elimu ya juu ya kiislam na wakristo kwa ngazi
ya vyuo vikuu vilivyoko katika chi za Kiarabu na nyingine ili kutafuta njia za pamoja
katika Taasisi za Kidini zilizo wazi katika kutafuta umoja na utamaduni na pia wepesi
wa kuhamasisha wema wa haki ya kila mzalendo.
Mtandao huo unaunganisha wanachama wa Taasisi ya elimu ya juu ya Chuo Kikuu zenye kuwa na matawi yake katika nchi za uarabuni, lakini miongoni mwao kuna hata chuo cha Kiislam cha Sharia na mafunzo ya Kiislam(College of Sharia and Islamic Studies) Qatar; Chuo Kikuu cha Sheria nchini Jordania; Taasisi ya chuo Kikuu cha Kidomeincani cha masomo ya Mashariki kilichopo Mjini Cairo. Tawi la Chuo Kikuu cha Masomo ya dini cha Notre Dame kilichopo Lebanon, Chuo Kikuu cha Ez-Zitouna (Tunisia, Chuo Kikuu cha Kiilsam Abdullah Bin Yassin (Mauritania) na Chuo Kikuu cha Kiinjili (Evangelical Theological Seminarry Cairo).
Wawakilishi wa taasisi wameweka lengo la kazi ya miaka mitatu ya mikutano na vikao vya kazi ili kupanua mpango kwa lengo la kuendeleza miongozo ilivyoainishwa katika siku ya mkutano huo. Ili kukabiliana na utata wa mtandao na kugundua vyombo vya habari na mitandao ya kijamii katika nafasi ya majadiliano na maelewano kwenye utambulisho tofauti, Kaiciid mwaka jana walifanya mjini Amman mpango wa kwanza wa mafunzo kwa ajili ya wandesha sekta iitwayo Umoja dhidi ya vurugu kwa jina la dini. Kozi hiyo ya utafiti ilikuwa na lengo kubwa la kusambaza misingi na mikakati imara katika tovuti zenye kueneza na kuchochea chuki za kidini ili wapate kutambua ubora na wingi wa utamaduni na dini za Mashariki ya kati kama utajiri wa maisha ya binadamu na mshikamano.
Kituo cha Kaiciid kilifunguliwa mwaka 2012 huko Vienna nchini Austria; ambacho
pia kimeanzishwa Saudi Arabia, Hispania na Austria, kuna mwakilishi wa kudumu ambapo
pia wawakilisha wa madhehebu makubwa ya Wakristo, Budha, Wahindu, Wayahudi na Waislamu.
Diyar Consortium, ni shirika la kiekumene, kinachoendeshwa na Wakristo wa Kilutheri
kilichoanzishwa huko Bethlehemu mwaka 1995. Kinajiuhusisha na kushiriki katika programu
za kusaidia makundi yaliyoathirika zaidi kutoka nchi ya Palestina.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |